BUKOBA SPORTS

Sunday, October 25, 2015

JOSE MOURINHO NA CHELSEA KWENYE MATATIZO! JOSE ALIGOMA KUONGEA NA WANAHABARI, KLABU YAKE KUPIGWA FAINI!

Jose Mourinho!Jose Mourinho atajua nini litamkuta baada ya Siku chache kutoka kwa FA, Chama cha Soka England, baada ya Jana kupewa Kadi Nyekundu wakati Timu yake Chelsea ikifungwa 2-1 na West Ham huko Upton Park.
Mourinho aliadhibiwa na Refa Jon Moss wakati wa Haftaimu baada ya kudaiwa kutaka 'kuvamia' Chumba cha Waamuzi' wakati wa Mapumziko.
Wakati huo Chelsea ilishafungwa 1-0 na West Ham na kubaki Mtu baada ya Kiungo wao Nemanja Matic kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya Kadi za Njano 2 na pia Msaidizi wa Mourinho, Silvino Louro, kumfuatia Matic nje baada nae kupewa Kadi Nyekundu alipolalamika.
Katika Miezi ya hivi karibuni, Mourinho amekuwa akilalamika kuhusu yeye na Timu yake kusakamwa na Marefa.
Kauli hizo zilimfanya FA impige Faini Pauni 50,000 na kumpa Kifungo cha Mechi 1 asikanyage Uwanjani lakini Kifungo hicho kimesimamishwa kwa Mwaka Mmoja hadi Tarehe 16 Oktoba 2016 ili kumwangalia mwenendo wake.

Kutokana na Kadi Nyekundu ya Jana sasa FA watasubiri Ripoti ya Refa Jon Moss na kisha kuamua kama hili linastahili kumrejeshea Kifungo chake na Adhabu nyingine stahiki.
Vile vile, Mourinho Jana aligoma kuongea na Wanahabari baada ya Mechi ikiwa ni kinyume na Sheria za Ligi Kuu England lakini kwa kosa hili Klabu ndio hupigwa Faini.
Msimu huu, Chelsea, ambao ndio Mabingwa Watetezi, wameshafungwa Mechi 5 kati ya 10 za Ligi na wapo Nafasi ya 15.

No comments:

Post a Comment