Akiongea baada ya Mechi hiyo, Mourinho alieleza: “Nilimwacha Hazard kwa sababu tunaruhusu Goli nyingi. Lazima tujihami vizuri zaidi. Ukiwa huna Mpira, kipaji chako hakina maana!”
Mourinho aliongeza: “Willian na Pedro walicheza vizuri katika kujihami na kuwapa nafuu Viungo wa kati. Hazard atakuwa nje hadi atakapoweza kutoa mchango katika kujihami kama wanavyofanya Willian na Pedro.”
Mechi hiyo Jana ni ushindi wa 3 tu kwa Chelsea, ambao ni Mabingwa Watetezi wa England, katika Ligi Kuu England Msimu huu na sasa wamepanda hadi Nafasi ya 11 wakiwa na Pointi 11 kwa Mechi 9 na wapo Pointi 10 nyuma ya Vinara Man City.
No comments:
Post a Comment