Dakika ya 64 pasi ya Juan Mata ilimkuta Marcus Rashford aliefunga na kuwapa Man United uongozi wa Bao 2-1.
Dakika ya 75, si mwingine tena bali Kijana mpya wa Kitaa, Marcus Rashford, aliepiga Bao la 3 kwa kuunganisha Krosi ya Varela.
Herrera aliipa Man United Bao la 4 kwa Penati katika Dakika ya 88 na Memphis kushindilia Bao la 5 Dakika ya 90.
Man United sasa wamesonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na watamjua mpinzani wao Kesho Ijumaa Februari 26 baada ya Droo itakayofanyika huko Nyon, Uswisi.
Marcus Rashford dakika ya 63 aliipatia bao Man United kwa kufanya 2-1. Bila kutegemewa Kijana wa Miaka 18, Marcus Rashford, aliekuwa kapangwa Benchi alilazimika kuanza Mechi hii na hakutetereka kwa kuifungia Manchester United Bao 2 walipoishindilia FC Midtjylland Bao 5-1 na kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI kwa Jumla ya Bao 6-3 baada ya kupoteza Mechi ya kwanza 2-1.
Kabla ya Mechi kuanza Man United walipata pigo kubwa baada ya Anthony Martial, ambae alipangwa kuanza Mechi hii, kuumia wakati akipasha moto na nafasi yake kuchukuliwa na Chipukizi Marcus Rashford ikiwa Mechi yake ya kwanza kabisa kuchezea Timu ya Kwanza.
Pigo hilo lilifanya Benchi la Akiba la Man United kubakia na Wachezaji wa Akiba 6 tu kwenye Benchi badala ya wale 7 wanaotakiwa kuwepo.
FC Midtjylland walitangulia kufunga Dakika ya 28 kwa Bao la Pione Sisto lakini Dakika 4 baadae Bodurov alijifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa Krosi ya Memphis.
Dakika ya 42 Man United walipewa Penati kutokana na Andre Romer kumuangusha Herrera lakini Juan Mata alipiga mkwaju wa Penati hiyo kidhaifu na Kipa Andersen kuokoa.
Manchester United bao lake limefungwa na Nikolay Bodurov dakika ya 32 likiwa ni bao la kuifunga wao wenyewe FC Midtjylland.
FC Midtjylland bao limefungwa na Pione Sisto dakika ya 27Paul Scholes
Martial aumia wakati anapashaManchester United vs Midtyjylland LIVE: Europa League
VIKOSI:
MANCHESTER UNITED XI: Romero; Varela, Carrick, Blind, Riley; Schneiderlin, Ander Herrera; Lingard, Mata, Memphis; Martial
AKIBA: J. Pereira, Rojo, Poole, McNair, Love, A. Pereira, Rashford
MIDTJYLLAND XI: Andersen, Rømer, Hansen, Bodurov, Novak, Sparv, Poulsen, Olsson, Hassan, Sisto, Urena
AKIBA: Dahlin, Banggaard, Bach Bak, Royer, Pusic, V. Kadlec, Onuachu
No comments:
Post a Comment