Barcelona waliwachapa Mtu 10 Real Betis 2-0 huku Timu zinazoikimbiza kileleni Atletico Madrid na Real Madrid zikishinda 1-0 kila mmoja.
Bao za Barca hiyo Jana zilifungwa na Ivan Rakitic na Luis Suarez katika Dakika za 50 na 81 dhidi ya Real Betis iliyobaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 35 baada ya Heiko Westermann kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano 2.
Nao Atletico walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano kwa Bao la Antoine Griezman huku Real, wakicheza Ugenini, wakiitungua Real Sociedad 1-0 kwa Bao la Gareth Bale.
Hiyo Jana Real ilicheza bila ya Mastraika wao Cristiano Ronaldo na Karim Benzema ambao ni Majeruhi. Huku zikibaki Mechi 2 Barca wapo kileleni wakiwa na Pointi 85 sawa na Atletico lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli. Real wapo Pointi 1 nyuma yao.
No comments:
Post a Comment