BUKOBA SPORTS

Sunday, May 1, 2016

LEO NI MANCHESTER UNITED vs LEICESTER CITY NDANI YA OLD TRAFFORD, NANI KUIBUKA KIDEDEA?

MENEJA wa Leicester City ameitaka Timu yake kumaliza Msimu wao wa BPL, Ligi Kuu England mithili ya sinema ili kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Miaka 132 ya Historia yao watakapocheza hii Leo Uwanjani Old Trafford na Manchester United.
Ikiwa Leicester watashinda hii Mechi basi watakuwa Mabingwa huku wakiwa na Mechi 2 mkononi kwani Timu ya Pili Tottenham haiwezi kuwakamata.
Ranieri ameeleza: "Huwezi kuamini, ni historia na tunajua hilo. Ni muhimu kumaliza hadithi hii kama Sinema ya Kimarekani. Mwisho mwema!"

Man United v Leicester City
-Man United wamefungwa Mechi 1 tu kati ya 13 za mwisho dhidi ya Leicester na hiyo ilikuwa 5-3 Msimu uliopita huko King Power Stadium.
-Mechi ya mwisho kati ya Leicester na Man United ilichezwa Novemba 28 huko King Power Stadium na kuisha 1-1.
-Leicester, ambao wako kileleni mwa BPL kwa Siku zaidi ya 100, wamefungwa Mechi 1 tu kati ya 13 zilizopita.

No comments:

Post a Comment