BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 20, 2016

TIMU YA BAYERN MUNICH YAKALIBIA KUBEBA TREBO!

KOCHA MKUU wa Bayern Munich Pep Guardiola amefurahia ndoto yao ya kutwaa Trebo Msimu huu kuwekwa hai baada ya Jana kuitwanga Werder Bremen 2-0 na kutinga Fainali ya Kombe la Germany, DFB POKAL.
Kwenye Mechi hiyo iliyochezwa Mjini Munich kwenye Uwanja wa Allianz Arena Bao 2 za Thomas Muller za Dakika za 30 na Penati ya Dakika ya 71 ndizo ziliwapa ushindi Bayern wa 2-0.
Mbali ya kuwa na hakika kubwa ya kutetea vyema Taji lao la Ubingwa wa Germany la Ligi ya Bundesliga, Bayern pia wapo Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ambao baadae Mwezi huu wataivaa Atletico Madrid ya Spain.
Kwenye Fainali ya DFB POKAL, Bayern watakumbana na Mshindi kati ya Hertha Berlin na Borussia Dortmund watakaocheza Leo huko Olympiastadion Jijini Berlin.

No comments:

Post a Comment