Hii pia ni mara ya kwanza kwa Liverpool kutinga Fainali ya Ulaya na kuwania Taji kwa Miaka 11.
Wakati Sevilla chiki ya Kocha Unai Emery inategemea sana ufungaji wa Mfaransa Kevin Gameiro ambae Msimu huu amepiga Bao 7 kwenye EUROPA LIGI, Liverpool hutegemea sana ubunifu wa kutengeneza Magoli na kufunga wa Mbrazil Philippe Coutinho.
Wakati Sevilla ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili kwa kulitwaa mara 2 mfululizo huku wakisaka kulitwaa mara ya 3 na kuwa Klabu ya kwanza kufanya hivyo, Liverpool, chini ya Meneja wao Jurgen Kloop ambae yuko Klabuni hapo kwa Miezi 7 tu, wanasaka mafanikio katika Fainali ya pili Msimu huu baada ya Mwezi Februari kushindwa kwa Penati na Man City kwenye Fainali ya Capital One Cup.
Liverpool wanategemea Divock Origi kupona Enka yake aliyoumia Aprili na Kepteni wao Jordan Henderson anaweza kucheza baada ya Juzi kucheza kwa Dakika 27 za Mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu England walipotoka Sare na WBA kufuatia kupona kwake maumivu yake.
Lakini Liverpool itamkosa Sentahafu wao Mamadou Sakho ambae amefungiwa Siku 30 kupisha uchunguzi wa kutumia Madawa Marufku kwa Wanamichezo.
Sevilla itawakosa Wachezaji wao Wawili, Michael Krohn-Dehli, ambae ameumia Goti na Jose Antonio Reyes ambae ni Mgonjwa na hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa Tumbo lake.
No comments:
Post a Comment