Bao la 100 la Wayne Rooney kwenye Uwanja wa Old Trafford, Thierry Henry To ndie anaongoza ana bao 114! Young dakika ya 87 aliifungia bao la 3 na kufanya 3-0 baada ya kuwachomoka mabeki wa Bournemouth akitupiwa pasi na Nohodha Wayne Rooney kwa juu. Dakika ya 90 Beki Smalling alijifunga bao kwa kujichanganya na wenzake dakika ya 90 na kuufanya mtanange kumalizika kwa bao 3-1.
Ushindi huu unawapandisha nafasi ya 5 Man United wakilingana pointi 66 sawa na Man City wakitofautiana ubora wa Mabao tuu. Siku nne zijazo Man United ataumana na Crystal Palace kwenye Fainali ya FA Cup.
Rooney akipongezwa kwa bao alilolifunga kipindi cha kwanza, Dogo Rashford alifunga bao la pili na kufanya 2-0 dhidi Bournemouth dakika ya 74.
Rooney 1-0
Man United sasa wako mbele kwa bao la Kepteni wake Wayne Rooney na likiwa bao lake la 100 kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Wayne Rooney dakika ya 43 anaipachikia bao la kuongoza 1-0 dhidi ya Timu ya Bournemouth.
Valencia akiendesha mpira
Hadi Mapumziko Manchester United 1 Bournemouth 0


VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Borthwick-Jackson, Carrick, Mata, Lingard, Rooney, Martial, Rashford
Akiba: Jones, Depay, Young, Romero, Ander Herrera, Varela, Andreas Pereira
Bournemouth: Federici, Francis, Elphick, Cook, Daniels, Ritchie, Gosling, Surman, Pugh, Wilson, King
Akiba: Gradel, Stanislas, Afobe, Grabban, O'Kane, Holmes, Jordan
Refa: Jon Moss
No comments:
Post a Comment