
Kufuatia Kura za Wanahabari 290, Asilimia 36 ilimpa Vardy na kuwabwaga wenzake wa Leicester, Riyad Mahrez na N'Golo Kante, waliokuwa wakichuana nae.
Vardy, mwenye Miaka 29, amefunga Bao 29 Msimu huu kwa Klabu yake na England na kuiongoza Leicester kuchungulia Ubingwa wa BPL, Ligi Kuu England.
Mbali ya Vardy, Mahrez na Kante, Wachezaji wengine wa Leicester waliokuwemo kwenye kinyang’anyiro cha Kura za FWA ni Danny Drinkwater, Kasper Schmeichel, Wes Morgan na Danny Simpson.
Vardy atatunukiwa Tuzo yake hapo Mei 12 kwenye Hafla maalum Jijini London.
Tuzo hii ya FWA imekuwa ikitolewa kila Mwaka kuanzia 1948/
No comments:
Post a Comment