Kwenye tukio hilo, Huth alimvuta Nywele Fellaini na Kiungo huyo wa Man United kulipiza hapo hapo kwa kumpiga na kiwiko na vitendo hivyo havikuonwa na Refa Michael Oliver.
Ikiwa watafunguliwa Mashitaka ya Uchezaji wa Fujo, Wachezaji hao wapo hatarini kupata Kifungo cha Mechi 3 kila mmoja na hili litamaanisha Msimu wao wa Ligi ndio umekwisha.
Lakini kwa sababu Man United wamebakiza Mechi 3 za Ligi na Leicester 2 tu, Fellaini anaweza kucheza tena Msimu huu kwenye Fainali ya FA CUP hapo Mei 21 dhidi ya Crystal Palace.
No comments:
Post a Comment