BUKOBA SPORTS

Thursday, December 22, 2016

MKHITARYAN AZOA TUZO MCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA MARA YA 6 MFULULIZO!

KIUNGO wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan Leo amezoa Tuzo yake ya 6 mfululizo kama Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yake Armenia.
Hii ni Tuzo yake ya 7 tangu avuke Umri wa Miaka 20 na kumfanya awemo kwenye Rekodi za Mastaa wa Dunia waliozoa mara nyingi Tuzo za aina hiyo.
Anaeongoza kwa Tuzo aina hii kwa Nchi yake ni Mchezaji mwenzake Mkhitaryan huko Man United, Zlatan Ibrahimovic, ambae amechukua mara 11.
Wengine wanaomkimbiza Ibrahimovic ni Wachezaji toka Finland, Sami Hyypia, alietwaa mara 9 na Jari Litmanen, mara 8, na Kipa wa Czech Republic Petr Cech mara 8.

Lakini hao wote wamestaafu Timu za Taifa wakati Mkhitaryan bado anacheza akikimbizwa kwa karibu na wale ambao bado wanadunda Timu zao za Taifa kina Gareth Bale wa Wales na David Alaba wa Austria, wote wakiwa na Tuzo 6 kila mmoja.

Wengine waliowahi kutwaa Tuzo 6 enzi zao ni Andriy Shevchenko wa Ukraine na Aliaksandr Hleb wa Belarus.

Walotwaa mara 5 ni Marek Hamsik (Slovenia), Robert Lewandowski (Poland), Goran Pandev (Macedonia) na Mstaafu Kakha Kaladze (Georgia).

Kwenye baadhi ya Nchi Tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka zina mifumo tofauti kama vile Portugal ambako zipo za aina mbili za yule achezae Ligi ya ndani na yule achezae nje ya Nchi.

Huko, kwa Wachezaji wa nje, Cristiano Ronaldo amezoa mara 8 katika Miaka 10 iliyopita.

Na Argentina wana mfumo wa aina hiyo hiyo ingawa kabla haijabaguliwa Lionel Messi alibeba Tuzo mara 2 na ilipotofautishwa kati ya Wachezaji wa ndani na nje, Messi alipewa mara 8 kati ya 9 kwa wa nje tangu wakati huo.

No comments:

Post a Comment