EPL, ambayo sasa imeshachezwa Mechi 19 kati ya 38 za Msimu mzima, inaongozwa na Chelsea wenye Pointi 49 wakifuata Liverpool wenye 43, kisha Arsenal wenye 40 na kufuatia Tottenham na Man City zenye 39 kila mmoja huku ya 6 ikiwa Man United yenye Pointi 36.
Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud kwa Kisigino katika Dakika ya 17 na kudumu hadi Mapumziko.
Arsenal wakapiga Bao la Pili Dakika ya 56 kupitia Alex Iwobi.
Katika Mechi ya kwanza ya EPL iliyochezwa hii Leo, Harry Kane na Dele Alli alipiga Bao 2 kila Mtu wakati Tottenham ikiwatwanga Watford waliodorora 4-1 na kutinga kwenye 4 Bora ya EPL kwamara ya kwanza tangu Oktoba.
EPL itaendelea tena Kesho Jumatatu kwa Mechi 6.
No comments:
Post a Comment