BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 26, 2017

EPL: CHELSEA YAWATWANGA SOUTHAMPTON BAO 4-2, WANUSA UBINGWA SASA!


LIGI KUU ENGLAND, EPL, imeendelea Jana kwa Mechi moja wakati Vinara Chelsea wakiwa kwao Stamford Bridge walipoitwanga Southampton, maarufu kama Watakatifu, Bao 4-2 na kwenda Pointi 7 juu kileleni.
Wakitoka kufungwa 2-0 na Man United katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi, Chelsea waliongoza 2-1 hadi Haftaimu kwa Bao za Eden Hazard na Gary Cahill huku Southampton wakipata Bao lao kupitia Mfungaji Oriol Romeu.
Kipindi cha Pili, Diego Costa akapiga Bao 2 na Chelsea kuongoza 4-1 lakini Southampton wakafunga Bao lao la Pili mwishoni Mfungaji akiwa Ryan Bertrand na Gemu kwisha 4-2.

Leo zipo Mechi 3 ambazo huko Emirates ni Arsenal na Mabingwa Watetezi Leicester City wakati Riverside ni Middlesbrough na Sunderland na huko Selhurst Park ni Crystal Palace na Tottenham Hotspur.
Alhamisi kazi kubwa ipo huko Etihad ambako iko Dabi ya Jiji la Manchester kati ya Man City na Man United Timu ambazo zinapishana Pointi 1 tu wakati City wapo Nafasi ya 4 na Man United Nafasi ya 5.

No comments:

Post a Comment