
Ikicheza zikiwa zimepita siku mbili tangu watoke sare tasa na Crystal Palace, City walipata goli lao kwa kwanza katika dakika 38 likiwa goli la mapema mno kupitia kwa Raheem Sterling akitumbukiza kimiani mpira wa krosi ya Leroy Sane.
Manchester City ilipata goli la pili baada ya Christian Kabasele kujifunga akijaribu kuokoa krosi ya Kevin de Bruyne, Sergio Aguero akafunga la tatu na kisha Andre Gray akafunga goli la kufutia machozi katika dakika za mwisho.


No comments:
Post a Comment