Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi ya mpira wa Miguu "Kamala Cup 2018" imefunguliwa leo Mjini Bukoba kwenye Uwanja wa Kaitaba na kushuhudia Timu ya Bakoba ikichapwa bao 2-0 na Timu ya Kahororo. Bao la kwanza la Timu ya Kahororo Fc lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 80 na Juma Baezwa baada ya kuwachomoka walinzi wa Timu ya Bakoba. Bao la pili lilifungwa dakika ya 83 na Jordan John na mtanange kumalizika kwa 2-0 dhidi ya wenyeji Baokoba Fc.
Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo ameipongeza timu hiyo kwa kuanza Ligi hiyo kwa ushindi pia amewataka Wananchi kuendelea kujitolea kuja kuzishabikia Timu za Kata zao na pia akiwashukuru kwa kujitokeza kwa Wingi kama walivyoingia leo kwenye Uzinduzi. Ligi hii ilikuwa ianze siku ya Alhamisi lakini ilisogezwa mbele kutokana na michezo ya Ligi kuu Vodacom inayeondelea hivi sasa. Mdhamini ametaja zawadi za Washindi katika Ligi hiyo kuwa wa kwanza atazawadiwa kitita cha Tsh. Milioni mbili(2) na Mshindi wa Tatu atapatiwa kitita cha Milioni 1 na nusu huku mshindi wa tatu akijinyakulia kiasi cha milioni moja. Ligi itaendelea tena kesho tarehe 19/02/2018 na kuzikutanisha Timu ya Vetran Bkb vs Ijuganyondo na Bilele vs Rwamishenye.
Wakati wa Mapumziko Ngoma ilipamba Moto.
Kipindi cha pili kiliendelea....Kipa wa Bakoba Fc akikimbilia mpira...
Wadau wakitazama mpira
Bao la pili lilifungwa na Jordan John dakika ya 83 na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Timu ya Bakoba Fc.
Raha ya bao...
2-0
Kulia kiongozi wa Timu ya Kahororo nae alisogea kuwapongeza Wachezaji wake kwa kuanza kwenye Ligi hiyo huku dakika zikiwa zimeyoyoma.
Mpaka dakika 90 zinakamilika Bakoba Fc 0 Kahororo 2.
No comments:
Post a Comment