BUKOBA SPORTS

Monday, February 19, 2018

KAMALA CUP 2018: VETRAN BUKOBA 1 vs 2 IJUGANYONDO FC, KAPIRIMA NA EDGAR WAIPA USHINDI IJUGANYONDO FC LEO KAITABA.

Ligi ya Kamala Cup 2018 imeendelea tena leo na Timu ya Veteran Bukoba wamenyukwa bao 2-1 na Timu ya Ijuganyondo. Bao la kwanza lilifungwa na Kapirima yusuph kipindi cha kwanza na bao la pili lilifungwa kipindi cha pili na Edgar Biazo huku bao la pekee la Timu ya Veteran BKB likifungwa na Shamte Odiro kipindi cha kwanza.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Ijuganyondo Fc Kata ambayo anatokea Mdhamini wa Ligi hii Kamala wakiomba mara baada ya kumaliza Mchezo wao na kuibuka kidedea kwa bao 2-1 dhidi ya Vetrani BKB kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Punde leo hii.
Kapirima Yusuph(kulia) akiwapongeza wachezaji wenzake leo hii kwa ushindi huku yeye akiwa kafunga bao moja kwenye mawili yaliyopatikana.
Wafungaji wa Ijuganyondo Fc Edgar Biazo (kulia) na Kapirima Yusuph (kushoto).
Mtanange unaendelea kwa sasa ni Bilele Fc Vijana wanaojulikana kutoka Kilomita 0 mjini Bukoba Katikati wakicheza na Rwamishenye FC. Rwamishenye tayari wanaondoza bao 2-0 mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment