TIMU ya Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Azam FC na kufikisha 34 sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.
Kagera Sugar yenyewe inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi 18 na sasa inajinasua mkiani ikirudi nafasi ya 15 kwa wastani wa mabao tu baada ya kulingana kwa pointi na Njombe Mji FC.
Katika mchezo wa leo, Kagera Sugar walitangulia kwa bao la beki Eladslaus Mfulebe dakika ya 50, kabla ya Iddi Kipagwile kuisawazishia Azam FC dakika ya 53.
Kikosi cha Azam FC: Kipa Razack Abalora, Saleh Abdallah/Iddi Kipagwile dk46, Bruce Kangwa, David Mwantika, Yakub Mohammed, Abdallah Kheri, Stephan Kingue/Paul Peter dk74, Frank Domayo, Salmin Hoza, Mbaraka Yussuph/Ennok Atta Agyei dk46 na Shaaban Idd.
Shangwe kwa Kagera Sugar, wameumaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Timu ya jijini Dar es salaam Azam Fc.
Kikosi cha Timu ya Azam Fc kilichoanza leo dhidi ya Kagera Sugar.
Mchezaji wa Azam Fc Kangwa(kulia) akipanga namna ya kumtoka mchezaji wa Kagera Sugar leo kwenye Uwanja Kaitaba leo. Picha zote na Faustine Ruta
Kagwa tena...
Mshambuliaji wa Azam Fc Mbaraka Yusuph akigombea mpira
No comments:
Post a Comment