Lakini Mancini hataki kuimarisha Difensi tu pia anamwinda Winga wa Tottenham Gareth Bale na pia anahusishwa na Mchezaji wa Argentina Matias Rodriguez ambae hivi karibuni aliisaidia Klabu ya Chile Universidad de Chile kutwaa Copa Sudamericana Kombe ambalo kwa Marekani ya Kusini ni sawa na EUROPA LIGI ya Barani Ulaya.
Ikiwa Coloccini na Rodriguez watafanikiwa kutua Man City basi wataungana na Wachezaji wengine kutoka Argentina ambao wako hapo kina Carlos Tevez, Sergio Aguero na Pablo Zabaleta.
Huko Spain, Kocha wa Vigogo FC Barcelona, Tito Vilanova, ameambiwa ana dau la Euro Milioni 25 tu kununua Wachezaji kwa ajili ya Msimu ujao pamoja na kitita kingine chochote kitakacho patikana akiuza Wachezaji.
Msimamo huo unaleta hatihati kwa Wachezaji wakongwe Seydou Keita, Adriano, Ibrahim Afellay na Dani Alves ambao wanadhaniwa ndio wataingizwa Sokoni.
Wakati huo huo, Barca imefuta Mkataba wao na Beki toka Brazil Henrique ambae alinunuliwa kwa Euro Milioni 8 Mwaka 2008 toka Palmeiras na kupewa Mkataba wa Miaka mitano lakini kwa Miaka minne amekuwa nje kwa mkopo.
Mara baada ya kununuliwa na Barca alipelekwa kwa mkopo Bayer Leverkusen kwa Mwaka mmoja, kisha kwenda Racing Santander kwa Miaka miwili na Julai Mwaka jana akarudi Klabu yake Palmeiras kwa mkopo wa Mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment