BUKOBA SPORTS

Friday, September 7, 2012

SIMBA YAPATA KICHAPO CHA MABAO 3-0 KUTOKA KWA SOFAPAKA YA KENYA


Mshambuliaji wa Simba, Edward Christopher akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Sofapaka ya Kenya , Anthony Kimani katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Sofapaka ilishinda 3-0.
MABINGWA wa Tanzania, Simba walishindwa kukonga nyoyo za mashabiki wao baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Sofapaka ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabingwa hao wa zamani wa Kenya, Sofapaka walitalawa sehemu kubwa ya mchezo huo na kufanikiwa kupata mabao yao kupitia kwa John Baraza aliyefunga mabao mawili na Joseph Nyanga.
Ochieng amesajiliwa kutoka AFC Leopard ya Kenya, Keita kutoka Stella Abidjan ya Ivory Coast na Akuffo kutoka Hearts Of Oak ya Ghana na wote hawajawahi kucheza Uwanja wa Taifa, hivyo leo ilikuwa mara ya kwanza kwao.
Simba, ambayo mara ya mwisho Simba ilicheza Dar es Salaam Agosti 8, na kufungwa mabao 3-1 na City Stars ya Nairobi, Kenya Uwanja wa Taifa, kwa zaidi ya mwezi mmoja ilikuwa kambini Arusha ikijifua vikali kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao wao ni mabingwa watetezi.
Kwa sasa kiwango cha Simba, inayofundishwa na Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick, akisaidiwa na Mganda, Richard Hamatre, kipo vizuri na timu inaonekana iko tayari kwa Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment