BUKOBA SPORTS

Sunday, November 4, 2012

ENGLISH PREMIER LEAGUE: SARE IMECHANGIWA NA MECHI NGUMU ZA UNITED - DI MATTEO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Roberto Di Matteo amesema kuwa sababu kubwa ya kikosi chake kutoa sare katika mchezo dhidi ya Swansea ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na michezo migumu miwili dhidi ya Manchester United. Katika mchezo dhidi ya Swansea ambao ulichezwa jana Chelsea walijikuta wakiruhusu wavu wao kutikiswa katika dakika ya 88 na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa sare. Lakini Di Matteo alitoa malalamiko yake kwa Chama cha Soka nchini Uingereza kufuatia tuhuma za lugha mbovu iliyotumiwa na mwamuzi Mark Clattenburg dhidi ya kiungo wake John Mikael Obi katika mchezo dhidi ya United. Katika mchezo huo uliochezwa Jumapili Iliyopita ambao United ilishinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Chelsea katika Uwanja wa

Torres alishindwa kuonesha tena cheche zake.
Stamford Bridge Clattenburg anatuhumiwa kumtolea maneno ya kibaguzi Mikael Obi.Di Matteo akifatilia mtanange jana.

________________________________________________



VETTEL DISQUALIFIED AT ABU DHABI GRAND PRIX.

 DEREVA nyota wa Langalanga, Sebastian Vettel ameshindwa kufuzu kuanza mwanzoni katika michuano ya Abu Dhabi Grand Prix ambapo sasa itabidi aanze mashindano hayo katika mstari wa nyuma. Vettel ambaye anaongoza orodha ya madereva bora msimu huu alimaliza mazoezi ya mashindano hayo akiwa watatu lakini alinyang’anywa nafasi hiyo baada ya gari lake kushindwakubakisha mafuta kwa ajili ya vipimo. Vettel alisimamisha gari lake pembeni wakati akirejea baada ya kumaliza mbio hizo baada ya kuishiwa mafuta katika tukio lililowahi kumtokea pia dereva wa McLaren Lewis Hamilton nchini Hispania Mei mwaka huu. Hatua hiyo itampa nafasi mpinzani wake katika mbio za ubingwa msimu huu Fernando Alonso wa timu ya Ferrari kumkaribia Vettel ambaye anaongoza kwa tofauti ya alama 13 katika msimamo wa madereva bora msimu huu.Alonso remains behind Vettel in the race for the drivers' titleDriving through the pack: Sebastian Vettel started at the back of the grid
Driving through the pack: Sebastian Vettel started at the back of the gridClash: Force India's Nico Hulkenberg, Paul di Resta and Sauber's Sergio Perez touch wheels after the start of the raceOff track: Nico Hulkenberg crashes with Bruno Senna
Nico Hulkenberg crashes with Bruno SennaOff and running: Lewis Hamilton made an impressive start from pole position
 Lewis Hamilton made an impressive start from pole position

source:dailymail

No comments:

Post a Comment