BUKOBA SPORTS

Sunday, November 4, 2012

SIRIE A:REKODI YA JUVE KUTOFUNGWA YAULIWA JANA, YACHAPWA 3-1 NA INTER MILAN. LA LIGA: BARCA NA REAL ZASHINDA

Ligi mbalimbali za Ulaya zimeendelea na huko Italy, ile rekodi ya Mabingwa wa huko Juventus ya kutofungwa katika Mechi 49 za Serie A jana ilimalizika katika Mechi yao ya 50 walipochapwa na Inter Milan Bao 3-1.Juventus, wakicheza nyumbani, walitangulia kupata bao katika Dakika ya kwanza tu kwa Bao la Arturo Vidal lakini Inter Milan walicharuka na kupata bao zao zote Kipindi cha Pili wafungaji wakiwa Diego Milito, Dakika ya 59 kwa Penati na bao lake jingine katika Dakika ya 75 na la tatu kufungwa na Palacio katika Dakika ya 90.

MATOKEO:
LA LIGA
Malaga 1 Rayo Vallecano 2
Barcelona 3 Celta Vigo 1
Real Madrid 4 Real Zaragoza 0
Valencia 2 Atletico Madrid 0

SERIE A
AC Milan 5 Chievo Verona 1

BUNDESLIGA
Hoffenheim 3 Schalke 2
Hannover 2 Augsburg 0
Borussia Monchengladbach 1 Freiburg 1
Nuremberg 1 Wolfsburg 0
Borussia Dortmund 0 Stuttgart 0
Hamburger 0 Bayern Munich 3


Huko Spain, Barcelona na Real Madrid zote zilishinda Mechi zao za nyumbani lakini katika Mechi hizo si Lionel Messi wala Cristiano Ronaldo aliefunga bao kama ilivyo kawaida.
Bao za Barca katika ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Celta Vigo zilifungwa na Adriano, David Villa na Jordi Alba.
Nao Real Madrid waliichapa Real Zaragoza bao 4-0 na kuwafanya wapande hadi nafasi ya 3 na huo ulikuwa ushindi wa 100 kwa Meneja Jose Mourinho tangu aitwae Klabu hiyo.
Bao za Real zilifungwa na Gonzalo Higuain, Angel Di Maria, Michael Essien na Luka Modric.

No comments:

Post a Comment