Jumamosi itachezwa Mechi moja huko Emirates kwa Arsenal kuwakaribisha Everton lakini Jumapili zipo Mechi 3 na ya kwanza ni Mechi ya Timu za Daraja la chini ya Ligi Kuu England kwa Sheffield United kucheza na Charlton Athletic.
Mechi hiyo itafuatiwa na ile ya Klabu za Ligi Kuu England, Hull City na Sunderland.
Mechi ya mwisho ya Robo Fainali ni huko Etihad Jijini Manchester, ambayo ni Marudio ya Fainali iliyopita ya FA CUP kati ya Manchester City na Wigan, ambayo Wigan waliibuka kidedea Uwanjani Wembley kwa kuitungua Man City Bao 1-0 na kutwaa Kombe.
Mara baada ya Mechi hii, Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika.
FA CUP:RATIBA
ROBO FAINALI
Jumamosi Machi 8
15:45 Arsenal v Everton
Jumapili Machi 9
15:00 Sheffield United v Charlton
17:00 Hull City v Sunderland
19:05 Manchester City v Wigan
NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
FAINALI: Jumamosi Mei 17
No comments:
Post a Comment