MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester City, Samir Nasri amedai kuwa Yaya Toure angeheshimika zaidi kama angekuwa sio Mwafrika. Wachezaji walifunga mabao maridani ambayo yaliisaidia City kutoka nyuma na kuifunga Sunderland kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kunyakuwa Kombe la Ligi. Nasri na Yaya ToureLakini wakati akiulizwa ubora wa mchezaji mwenzake huyo, kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa alidai kuwa kutokana na ukweli kwamba Toure anatoka Ivory Coast hiyo inamfanya asipate heshima yake anayostahili. Nasri amesema kama Toure angekuwa sio Mwafrika kila mtu angesema ndio kiungo bora duniani kwasababu anaweza kufanya kila kitu, kufunga, kuzuia na kushambulia. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ni tofauti kwasababu anatokea Ivory Coast lakini kama angekuwa anatoka Argentina au Brazil kila mtu angekuwa na mzungumzia na wangeweza kulipa hata paundi milioni 40 au 50 kwa ajili yake.Yaya Toure akishangilia baada ya kutengeneza nafasi ya bao juzi kati ya City na Sunderland kwenye fainali ya Capital One CupNasri juzi alitupia la kiwango!
No comments:
Post a Comment