Mashabiki wa Liverpool walikusanyika kwa ajili ya Mechi hii wakiwa na hakika ya ushindi, hasa baada Jose Mourinho kudokeza atachezesha ‘Kikosi hafifu’, na kabla ya Mechi kuanza Basi lililobeba Wachezaji wa Liverpool lilipokuwa kwa shangwe kubwa nje ya Anfield mithili ya Paredi ya Ubingwa.
Bao zilizoiua Liverpool zilifungwa na Demba Ba katika Dakika ya 45 baada ya Nahodha Steven Gerrard kuteleza na Demba Ba kunufaika na kwenda kufunga na la Pili kupigwa Dakika za Majeruhi na Willian, alietokea Benchi, alipopokea Pasi murua ya Fernando Torres.
Ushindi huu umewaacha Chelsea wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Liverpool lakini huenda matokeo haya yakawanufaisha sana Manchester City ambao wana Mechi mbili mkononi na wakishinda zote wataikamata Liverpool na kuongoza kwa Ubora wao wa Magoli.
Mapenzi bado yapo!!! Kocha wa zamani wa Liverpool Kenny Dalglish akionesha kuchukia baada ya timu ya Liverpool kupoteza!!
No comments:
Post a Comment