BUKOBA SPORTS

Monday, April 28, 2014

LUIS SUAREZ ATWAA TUZO!! NI YA PFA-TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA. HAZARD NI MCHEZAJI BORA KIJANA! TIMU YA MWAKA: ARSENAL NA MAN UNITED NJE!!!!!!!

STRAIKA wa Liverpool Luis Suarez ametwaa Tuzo ya England ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya PFA [Professional Footballers' Association], Chama cha Wanasoka wa Kulipwa, hapo Jana.
Msimu uliopita, kipindi kama hiki, Luis Suarez alikuwa akianza kutumikia Adhabu ya Kifungo cha Mechi 10 baada kumuuma Meno Mchezaji wa Chelsea, Branislav Ivanovic, lakini safari hii ni kidedea.

Suarez alikabidhiwa Tuzo yake Jana Usiku kwenye Hoteli ya Kifahari, Grosvenor House, Jijini London mara baada ya kuruka kutoka Jijini Liverpool baada ya Mechi yao Uwanjani kwao Anfield walikofungwa Bao 2-0 na Chelsea.
All smiles: Suarez poses with Chelsea's Eden Hazard who scooped the award for Young Player of the Year
Msimu huu, Suarez amefunga Bao 30 katika Mechi 31 za Ligi licha ya kuzikosa Mechi za mwanzo wa Msimu akiwa bado Kifungoni.
Mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard, ambae hakucheza hiyo Jana huko Anfield, alitwaa Tuzo ya England ya Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka ya PFA.
Back of the net: Suarez fired Liverpool to the top of the Premier League as he scored against Tottenham
Kwenye Timu Bora ya Mwaka ya PFA ya Ligi Kuu England, Suarez alijumuika na wenzake wa Liverpool, Daniel Sturridge na Nahodha wao Steven Gerrard.
Chelsea pia walikuwa na Wachezaji watatu ambao ni Petr Cech, Gary Cahill na Hazard.
Gifted: The 23-year-old has netted 17 goals in all competitions from a deeper position this campaign
Manchester City inawakilishwa na Vincent Kompany na Yaya Toure huku Southampton ikiwa na wawili, Luke Shaw na Adam Lallana.
Mabingwa Watetezi, Manchester United nar Arsenal, haina hata Mchezaji mmoja.
Magician: Eden Hazard has been the one man to make Jose Mourinho's Chelsea tick this season
PFA-LIGI KUU ENGLAND-TIMU YA MWAKA:

 Petr Cech (Chelsea); Luke Shaw (Southampton), Vincent Kompany (Manchester City), Gary Cahill (Chelsea), Seamus Coleman (Everton); Eden Hazard (Chelsea), Yaya Toure (Manchester City), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Lallana (Southampton); Luis Suarez (Liverpool), Daniel Sturridge (Liverpool)

No comments:

Post a Comment