BUKOBA SPORTS

Thursday, May 1, 2014

EUROPA LEAGUE: JUVENTUS 0 v BENFICA 0 (Agg.1-2) MTANANGE WAMALIZIKA KWA SARE!! BENFICA WASONGA HATUA YA FAINALI KWA BAO LA UGENINI!!



BENFICA wamesonga hatua ya Fainali usiku huu baada ya kutoshana nguvu na timu ya Juventus kwa 0-0 leo kwenye uwanja wa Juventus Arena.
Juventus walihitaji Bao 1 ili kuibwaga nje Benfica waliporudiana leo mjini Turin, Italy kwenye dimba la Juventus Stadium na Benfica kusonga kwa Bao la Ugenini kwani waliifunga 2-1 katika Mechi ya Kwanza huko Lisbon wiki iliyopita.

Benfica pia walicheza mtanange huu kwa kuumaliza wakiwa pungufu baada ya kupata Pengo kwa katika dakika ya 67 Enzo Nicolás Pérez alipata kadi ya pili na kupewa kadi nyekundu.
Fainali ya EUROPA LIGI Msimu huu itachezwa Uwanjani kwa Juventus Stadium hapo Mei 14.
chupuchupu!!!PirloKocha akilalamika!
SAFARI YA TURIN:
NUSU FAINALI: Mechi Aprili 24 na Mei 1
FAINALI: Jumatano Mei 14, Juventus Stadium, Turin, Italy

No comments:

Post a Comment