SEVILLA Wamesonga hatua ya fainali baada ya mchezaji wake Stéphane M'Bia kufunga bao katika dakika za majeruhi dakika za nyongeza kipindi cha pili kwenye uwanja wa Estadio Mestalla.
Sevilla walishinda Mechi ya Kwanza kwa Bao 2 za Stephane MBia na Carlos Bacca na kuiacha Valencia ikiwa na mzigo mkubwa wa kushinda Mechi ya leo ya marudiano.
Valencia walijitahidi tangu mwanzo kwani waliweza kuzirudisha bao zote mbili na kufunga bao jingine la tatu na kujiona kwamba wameshinda kwa kishindo mchezo huu lakini kwa kuwa mpira ni dakika 90 dakika za nyongeza Sevilla waliweza kuziona nyavu na bao lao la pekee katika mtanange huu lilizaa matunda makubwa kwani limeweza kupindua kipigo cha bao 3-2 na kuwa sare ya 3-3 na hatimaye Sevilla kushinda kwa bao la Ugenini.
Bao la kwanza la Valencia lilifungwa Dakika ya 14 mchezaji wa Valencia Sofiane Feghouli aliifungia bao baada ya kupata pasi kutoka kwa Edu Vargas
Dakika ya 26 Beto anajifunga bao la pili na kufanya 2-0, Agg ikiwa ni 2-2.
Dakika ya 70 kipindi cha pili Jérémy Mathieu anaipachikia bao la tatu Valencia na kufanya 3-0 dhidi ya Sevilla waliokuwa mbele ya bao mbili za mechi ya kwanza.
Dakika za lala salama dakika ya 90 Sevilla wanapata bao lao la kufutia machozi huku likiwa ni neema kwao kwa kusawazisha kwenye Agg. ikiwa ni 3-3 kupitia kwa Stéphane M'Bia baada ya kupewa pasi na Federico Julián Fazio kwenye dakika za nyongeza.
Kwa ushindi huu Fainali itawakutanisha kati ya timu ya Sevilla na Benfica hapo Jumatano Mei tarehe 14 Turin mjini Itali.
No comments:
Post a Comment