BUKOBA SPORTS

Saturday, May 17, 2014

FA CUP LEO HII, BAADA YA MIAKA 9 ARSENAL WANA NAFASI MURUA KUMALIZA JANGA LAO LA UKAME DHIDI YA HULL CITY WEMBLEY STADIUM, LONDON, SAA 1 USIKU.

NAHODHA wa Hull City au Arsenal Leo Usiku Uwanjani Wembley Jijini London atabeba Kombe jipya kabisa la FA ikiwa Timu yake itaibuka kidedea kwenya Fainali ya FA CUP.
Image
Hii itakuwa ni mara ya 3 katika Historia ya Miaka 143 ya FA CUP kwa kwa FA, Chama cha Soka England, kulibadili Kombe la FA na mara nyingine ni kwenye Miaka ya 1911 na 1992.
Kombe hili jipya linafanana kabisa na lile Kombe la Mwaka 1911 na limebadilishwa baada ya kuchakaa.

Image
Kombe la zamani litabaki kwenye kumbukumbu za FA Uwanjani Wembley.
KWA WACHAMBUZI wengi huko Uingereza hii ni nafasi murua kwa Arsene Wenger na Arsenal yake kumaliza ukame wao wa Miaka 9 bila ya Kombe lolote wakati Jumamosi watakapoingia Wembley Stadium Jijini London kuivaa Hull City kwenye Fainali ya FA CUP.

Image
Arsenal wanapambana na Hull City ambao wamemaliza Msimu huu wakiwa Nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu England lakini kwa Meneja wa Hull City, Steve Bruce, Nguli wa Man United, faraja kubwa ni kukumbuka nini kiliwakuta Arsenal Miaka mitatu iliyopita walipotinga Wembley kwenye Fainali ya Kombe la Ligi na kuchapwa 2-1, bila kutarajiwa, na Birmingham City.Image
Wakiwa na Masupastaa kama kina Mesut Ozil, Santi Cazorla na Olivier Giroud, utabiri wote unanyoosha kidole kuwa Arsenal ndio Bingwa wa FA CUP na hasa ukizingatia Rekodi mbovu ya Hull City dhidi ya Arsenal ya kufungwa Mechi zote 2 za Ligi Kuu England Msimu huu na pia kutoifunga Arsenal tangu wakutane uso kwa uso kuanzia Mwaka 2009.
Arsenal leo wana nafasi ya kumaliza ukame wa miaka 9 kwa kutwaa kombe jipya la FA CupImageWenger anatarajiwa kufanya uamuzi nani amuweke Golini kati ya Kipa Lukas Fabianski, ambae amedaka Mechi zao zote za FA CUP Msimu huu, au Kipa Nambari Wani Wojciech Szczesny, ambae ametwaa Glovu za Dhahabu Msimu huu baada ya kuweka Rekodi ya kutofungwa katika Mechi 16 za Ligi Kuu England.Image

No comments:

Post a Comment