BUKOBA SPORTS

Saturday, May 17, 2014

MAN UNITED YAMSAINI KIPA KINDA WA SERBIA

MANCHESTER UNITED imekubaliana na Klabu ya Serbia, FK Vojovdina, ili kumsaini Kipa wao Chipukizi Vanja Milinkovic.
Milinkovic, Miaka 17, aling’ara mno akiidakia Serbia Mashindano ya Vijana ya UEFA U-17 na kuwafurahisha Man United baada ya kutofungwa Bao katika Mechi 3 kati ya 6.
Hata hivyo, Kipa huyo atabakia na Klabu yake FK Vojovdina kwa Msimu mmoja zaidi kabla hajahamia Old Trafford.

Wachezaji wengine waliowahi kuichezea Man United kutoka Nchini Serbia ni Nemanja Vidic na Zoran Tosic.

Milinkovic ni Mchezaji wa kwanza kuchukuliwa na Man United huku wakielekea kumthibitisha Meneja mpya wa Klabu hiyo, Louis van Gaal, ambae anatarajiwa kutangazwa Wiki ijayo na Wachezaji wengine wanaohusishwa kuhamia Old Trafford ni Mastaa waliojengeka kina Thomas Muller, Toni Kroos na Edinson Cavani.

No comments:

Post a Comment