Cristiano Ronaldo usiku huu ameisawazishia timu yake bao kutoka 2-1 na kuwa 2-2 kwenye mtanange uliopigwa wa kukata na shoka. Bao hilo lilipatikana katika dakika za majeruhi baada ya kupata krosi safi na kuimalizia vizuri kwa kisigino nyavuni mwa lango la Valencia.
Valencia ndio walianza kupata bao katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza kupitia kwa Jérémy Mathieu kwa kichwa safi huku Real wakisawazisha bao kipindi cha pili dakika ya 59 kupitia kwa Sergio Ramos.
Dakika ya 65 Daniel Parejo wa Valencia aliwachoma bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Real wenyeji. Bao la kusawazisha kwa kufanya 2-2 lilifungwa na Cristiano Ronaldo katika dakika za lala salama katika dakika ya 90 zikiwa zimeongezwa dakika 5 tuu.
2-1
Pisha!!
No comments:
Post a Comment