BUKOBA SPORTS

Sunday, May 11, 2014

MSAMA KUFUNGUA MADUKA MAJIJI MATANO

Na Mwandishi Wetu
IKIWA na lengo la kudhibiti wizi wa kazi za Sanaa hapa nchini, Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kufungua maduka katika majiji manne hapa nchini baada ya Dar es Salaam.
Kwa mjjibu wa Mkurugenzi wa kampni ya Msama Promotions, Alex Msama maduka hayo yatakuwa katika majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na mkoani Dodoma ambayo yatakuwa kazi halisi za wasanii.
Msama alisema kwa kuanzia wataanza na jiji la Mwanza, ambako wanatarajia kuweka duka katika mitaa ya Nyerere na Libert jijini humo.
Aidha Msama alisema mashabiki wengi wanauziwa DVD feki nyingi ambazo wanauziwa kati ya shilingi 1000-1500 ambazo zinadumu wii mbili wakati kazi halisi wanaziuza kwa bei ya jumla shilingi 2000 na rejareja shilingi 3000.
Msama alisema kwa jiji la Dar es Salaam, kampuni yake ina maduka katika maeneo ya Kariakoo mtaa wa Msimbazi naMasasi lingine lipo Posta Mpya mtaa wa Mkwepu

No comments:

Post a Comment