Blind, Miaka 24, alikuwemo kwenye Kikosi cha Louis van Gaal cha Timu ya Taifa ya Netherlands kilichocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil na alikuwa akichezeshwa kama Fulbeki wa Kushoto na Kiungo Mkabaji.

Dili hii itarajiwa kukamilika mara baada ya Mchezaji huyo kuafiki maslahi yake binafsi na upimwaji afya yake na atakuwa Mchezaji wa 5 kununuliwa na Man United katika Kipindi hiki cha Uhamisho.
Wachezaji wengine wapya wa Man United ni Angel Di Maria, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo.
Dirisha la Uhamisho la Wachezaji litafungwa Jumatatu Septemba Mosi na inatarajiwa Man United kusaini Wachezaji wengine wapya.
No comments:
Post a Comment