
Wachezaji wakisalimiana

Kikosi cha Geita Geita Gold SC ya mkoani Geita

Kikosi cha Kagera Sugar

Waamuzi wa mtanange huu kati ya Kagera Sugar na Geita
Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU Kagera Sugar imepambana na timu Geita Gold Sc ya Mkoani Geita ambayo iko daraja la kwanza jana jumapili (Agosti 31 mwaka huu) katika mechi ya majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba na timu ya Kagera Sugar kuibuka na Ushindi wa bao 1-0.
Timu ya Kagera Sugar ilipata bao kupitia kwa Mchezaji wake Salum Kanoni mapema dakika ya 7 kwa mpira wa adhabu baada ya kupigwa Frii kiki na kuziiliwa na Salum Kanoni kuumalizia mpira huo kwa shuti kali lililomzidi ujanja kipa wa Geita Gold Sc Emmanuel Sangra.

katika Mtanange huo kiingilio kilikuwa ni Tsh. 1,000 tu na Katika majaribio hayo ya Tiketi za Electoniki yalikwenda vyema katika Uwanja huo na Mashabiki waliingia kwa wingi na jambo hilo lilifanyika vyema kuanzia uuzwaji wa Tiketi hizo katika uwanja huo wenye kuingiza jumla ya Mashabiki 3,000.

Mchezaji wa timu ya Geita Gold SC Venas Joseph akilindwa kwa karibu na wachezaji wawili wa Kagera Sugar.

Erick Kyaruzi Mopa wa Kagera Sugar akiendesha mpira.

Steven Silvester wa Geita akituliza mpira huku akinyemelewa na Salum Kononi wa Kagera Sugar

Mchezaji wa Geita akiendasha mashambulizi kuelekea lango la Kagera Sugar.

Mtanange ukiendelea..

Abdurazack Mtanagazeji wa habari za Michezo wa Kituo cha Radio cha Kasibante Fm 88.5(kushoto) nae alikuwepo katika mtanange huo akichukua habari

Boniface Wambura, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)) akiwa meza kuu akishuhudia Mtanange huo uliochezewa kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Murage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar akiweka mambo sawa Uwanjani kutoa mchezaji na kumweka mwingine ili kuongeza nguvu.

Atupele na mpira....

Victor Hussein wa Kagera Sugar akimiliki mpira

Vuta nikutete...wakiwania mpira.

Mpira wa Kona ukisubiriwa kwenye lango la Geita Gold Sc

Albert malale wa timu ya Geita akiondosha mpira kwa staili yake

Mtanange ulimalizika Kagera Sugar wakiwa na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Salum Kanoni dakika ya 7 kipindi cha kwanza baada ya kupigwa mpira wa Adhabu wa frii kiki na kukingwa na Salum Kanoni kuachia shuti kali lililozama hadi langoni. Kumbuka mchezo huo ulikuwa ni wa kutesti tiketi za Electroniki na pia ukiwa ni mchezo wa kujipima huku Kagera Sugar ikikaribia kuanza kucheza Ligi kuu Bara Tanzania Vodacom sept. 20 ambapo wataanzia Ugenini Mjini Tanga.

Mpira ni furaha hapa kipa wa Geita Gold mine sport akisalimiana na wachezaji wawili wa Kagera Sugar.

Super Mkude Mwenyekiti wa Bukoba Veteran(kushoto) akiteta jambo na Wambura kwenye Uwanja wa Kagera Sugar mara baada ya mtanange huo kumalizika.

Mwenyekiti wa Bukoba Veteran, Supar Mkude akiwa na Kocha mkuu wa Kagera Sugar Jackson Mayanja ambaye ni raia wa Uganda, Wote wakiwa wamelamba Uzi wa Bukoba Veteran. Hakika itakuwa ni jambo la kumkaribisha kocha huyo katika klabu hiyo ya Bukoba Veteran.

Kocha wa Mkuu wa timu ya Geita Gold Sc ya Mkoani Geita Choki Abed akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kipute kumalizika kwa 1-0, Kagera wakiibuka na Ushindi kwenye Uwanja wao wa nyumbani Kaitaba.
No comments:
Post a Comment