BUKOBA SPORTS

Monday, October 6, 2014

CRISTIANO RONALDO APIGA HAT-TRICK! ATLETICO BILBAO WAKINYONGWA 5-0!

Cristiano Ronaldo, Jana alipiga Bao 3 wakati Real Madrid inaitwanga Athletic Bilbao Bao 5-0 kwenye Mechi ya La Liga iliyochezwa Santiago Bernabeu.
Msimu huu, Ronaldo ameshafikisha Bao 13 katika Mechi 6 na hii ni Hetitriki yake ya 3 kwa Msimu huu.Pia, sasa Ronaldo amefikisha Jumla ya Hetitriki 22 katika La Liga na kuifikia Rekodi inayoshikiliwa na Malejendari Alfredo Di Stéfano na Telmo Zarra wote wakiwa na Hetitriki 22 kila mmoja
Bao nyingine za Real hiyo Jana zilifungwa na Karim Benzema.
Ushindi huu umeifanya Real ikamate Nafasi ya 4 kwenye La Liga wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Barcelona
MATOKEO
Jumapili Oktoba 5

Sevilla FC 4 vs Deportivo La Coruna 1
Celta de Vigo 1 vs Villarreal CF 3
RCD Espanyol 2 vs Real Sociedad 0
Real Madrid CF 5 vs Athletic de Bilbao 0


No comments:

Post a Comment