BUKOBA SPORTS

Friday, October 3, 2014

RATIBA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII, JUMAMOSI MITANANGE 6 KUPIGWA! JUMAPILI NI PATASHIKA! MAN UNITED vs EVERTON, CHELSEA vs ARSENAL...

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:

Jumamosi Oktoba 4 
17:00 Hull v Crystal Palace
17:00 Leicester v Burnley
17:00 Liverpool v West Brom
17:00 Sunderland v Stoke
17:00 Swansea v Newcastle
19:30 Aston Villa v Man City 
Chelsea wapo kileleni na wakiwa na pointi 16
Jumapili Oktoba 5
14:00 Man United v Everton
16:05 Chelsea v Arsenal
16:05 Tottenham v Southampton
18:15 West Ham v QPR

Jumapili mechi ya kwanza na ya mapema ni Man United VS Everton mchezo utakaopigwa saa 8 mchana zikifuatiwa na mitanange miwili Chelsea na Arsenal pamoja na Spurs na Southampton.Mechi hiyo United watahitaji pointi tatu muhimu kwani wanachangamoto nafasi waliyopo 7 wakiwa wanafanana na timu 6 wenye alama 8 hivyo Alama tatu ni muhimu sana na watakuwa kwao Old Trafford. 

Van Gaal amesema: “Katika nafasi ya Rooney, Juan Mata ameshacheza vizuri sana. Inabidi nichague. Nitamkosa sana Rooney kwa sababu ni Nahodha lakini Mata anacheza vizuri sana nafasi hiyo.”
Kukosekana kwa Rooney Uwanjani kungeweza kumpa utepe wa Unahodha wa Mechi hii na Everton Darren Fletcher ambae ni Makamu wa Nahodha Man United kama atacheza lakini Van Gaal amekataa kuthibitisha hilo.
Van Gaal pia alitoboa kuwa anao Wachezaji 9 wa Timu ya Kwanza ambao ni Majeruhi ingawa wengine washaanza Mazoezi.
Van Gaal ameeleza: “Ni ngumu kueleza. Unaweza ukawa umepona lakini ukawa sio fiti kwa Mechi. Kwa mfano Herrera yuko fiti lakini hatakiwa kuguswa kwenye mbavu. Fellaini amefanya Mazoezi Wiki moja lakini hayuko fiti kucheza Dakika 90.”
JUAN MATA KUANZA MECHI YA LEO 
Aliongeza: “Tuna Masentahafu watatu majeruhi hivyo MacNair atacheza. Yeye ndio Mchezaji pekee anaeweza kucheza nafasi ya Kulia ya Sentahafu. Nilimchagua Mechi iliyopita na alicheza vizuri sana. Changamoto kubwa kwake ni kumudu kiwango kilekile.”
Kipa wa Man United De Gea

No comments:

Post a Comment