BUKOBA SPORTS

Saturday, November 8, 2014

BUNDESLIGA: THOMAS MULLER APIGA HAT-TRICK, BAYERN HAWASHIKIKI KILELENI!


Mabingwa Bayern Munich Leo wameishindilia Eintracht Frankfurt Bao 4-0 kwenye Bundesliga na kuzidi kuyoyoma kileleni.
Bao za Bayern zilifungwa na Thomas Muller Dakika za 22, 64 na 67 na la 4 na Xherdan Shaqiri kwenye Dakika ya 86.
Ushindi huu umezidi kuipaisha kileleni mwa Ligi hiyo ya Nchi ya Germany na sasa wana Pointi 27 kwa Mechi 8 wakifuatiwa na VfL Wolfsburg wenye Pointi 20.

Bao la kwanza limepatikana ndani ya dakika 22

Meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola akiteta na wachezaji wake Uwanjani.

Muller akifanya yake langoni

Thomas Muller akipongezana na Franck Ribery baada ya kutupia bao

Muller akimfunga bao la tatu kipa Felix Wiedwald

Mchezaji wa Bayern  Xherdan Shaqiri alitokea nje na kufunga bao la nne

Raha tupu!!! Xabi Alonso akimpongeza Thomas kwa kupiga hat-trick

No comments:

Post a Comment