BUKOBA SPORTS

Saturday, November 8, 2014

FULL TIME: YANGA 2 vs 0 MGAMBO JKT

Mpira ni Mapumziko hakuna timu iliyoliona lango la mwenzake! Yanga 0 - 0 Mgambo JKT.
Kipindi cha pili kinaendelea Yanga 0 - 0 Mgambo JKT
Saimon Msuva anaifungia bao Yanga na kufanya 1-0 dhidi Mgambo baada ya kupewa pasi na Mbuyu Twite katika dakika ya 73 huku Mgambo Jkt wakiwa pungufu baada ya Mwenzao kuoneshwa kadi nyekundu!
Zikiwa zimebaki dakika za nyongeza...
Yanga 2-0 Simon Msuva anaipachikia bao la pili Yanga na kufanya 2-0 dhidi ya Mgambo JKT na bao likifungwa dakika za lala salama dakika ya 90 kwa makosa ya Beki wa Mgambo na kipa wake na Msuva kuumalizia mpira langoni. Magoli yaote ya Yanga yakifungwa na Mchezaji mmoja Simon Msuva dakika ya 73 na 90.

No comments:

Post a Comment