BUKOBA SPORTS

Sunday, November 2, 2014

MANCHESTER CITY 1 vs 0 MANCHESTER UNITED

Wachezaji wa Man City wakishangilia na kupongezana kwa bao lililofungwa na Aguero dakika 63 kipindi cha pili.Aguero(kulia) akishangilia.
BAO la Dakika ya 63 la Sergio Aguero limewapa Manchester City ushindi wa Nyumbani kwao Etihad kwenye Dabi ya Jiji la Manchester walipoifunga Mtu 10 Manchester United kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Man United walibakia Mtu 10 kuanzia Dakika ya 39 wakati Sentahafu wao Chris Smalling alipotolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kupokea Kadi za Njano mbili.

Mbali ya pigo hilo, Man United walipata pigo jingine wakati Sentahafu wao mwingine Marcos Rojo kutolewa nje alipoumia Bega kwenye Dakika ya 56 na kuiacha Man United ina Difensi ya kuungaunga ya Antonio Valencia, Michael Carrick, Chipukizi wa Miaka 19 Paddy McNair na Luke Shaw.

Hii ilikuwa Mechi ya kwanza ya Ligi kwa Carrick tangu Msimu uanze baada ya kuumia enka.
Licha ya mapigo hayo ya Uwanjani, Man United pungufu ilicheza vizuri mwishoni na wangeweza kuambulia hata Sare.
Ushindi huu umeiweka Man City Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Southampton walio Nafasi ya 2 na Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea. Man United wamebaki Nafasi ya 8.
Smalling ameoneshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza mwishoni dakika 39Ni Shida kwenye lango la Man United.Yaya Toure chini!Kipa wa United De Gea bado ni shida...kwenye hii Debi!!Wayne Rooney arudi kwenye Debi ya Manchester United LEO Jumapili, Novemba 2, Uwanjani Etihad, Dabi ya Jiji la Manchester, Mechi inayongojewa na Mamilioni Duniani, itachezwa katika Mechi ya Ligi Kuu England wakati Wenyeji Manchester City watakapocheza na Mahasimu wao Manchester United.
Safari hii Man City wanatinga Uwanjani wakiwa ndio Mabingwa Watetezi na wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya Pili Southampton na Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.
Man United wao wako Nafasi ya 8 na wakiwa Pointi 4 nyuma ya Man City.

VIKOSI:
Manchester City:
Hart, Zabaleta, Kolarov, Demichelis, Kompany, Fernando, Yaya Toure, Navas, Milner, Jovetic, Aguero
Akiba: Caballero, Clichy, Sagna, Fernandinho, Boyata, Dzeko, Nasri
Manchester United: De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Fellaini, Januzaj, Rooney, Di Maria, van Persie
Akiba: Lindegaard, McNair, Carrick, Fletcher, Herrera, Mata, Wilson

No comments:

Post a Comment