Akiwa na Barcelona, Valdes alitwaa Ubingwa wa La Liga mara 6 na UEFA CHAMPIONS LIGI mara 3 na kabla Msimu uliopita kumalizika alitangaza kuondoka Barca baada ya mwenyewe kukataa kuongeza Mkataba wake.
Cambridge United, ambayo inacheza Ligi 2, ndio Timu pekee ya Daraja la chini kabisa iliyobakia kwenye Raundi ya 4 ya FA CUP na Mechi hii itakayochezwa Uwanjani kwao Abbey Stadium huko Cambridge ni ya Kihistoria kwao ingawa waliwahi kufika Robo Fainali ya FA CUP mara mbili katika Miaka ya 1990 na 1991.
wenye Msimamo wa Ligi 2, Cambridge United wako Nafasi ya 12.
No comments:
Post a Comment