
Kipre Tchetche alitumia dakika chache kuliona lango la Kagera Sugar
Wachezaji wa Azam Fc wakiyarudi Mangoma mara baada ya kupata bao lao la mapem Dakika ya 4 Kipindi cha kwanza cha dakika 45. Bao la pili lilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 38 kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili hich hicho Kona ilipigwa na Didier Kavumbagu alijitwisha kichwa na kufunga bao katika dakika ya 77 na kuipatia bao la tatu kwa kufanya 3-1 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.
Picha na Faustine Ruta wa Bukobasports.com
Hadi Mapumziko, Azam FC walikuwa mbele 2-0 ya Wenyejji wao Kagera Sugar ambao hivi sasa wanatumia CCM Kirumba kama Uwanja wa Nyumbani baada ya Kaitaba huko Bukoba kufungwa kwa ukarabati.
Bao za Azam FC zilifungwa na Kipre Tchetche na Didier Kavumbagu katika Kipindi cha Kwanza na Kipindi cha Pili Kagera Sugar wakapata Bao 1 kupitia Rashid Mandawa lakini ni tena Kavumbagu akawahakikishia ushindi kwa kupiga Bao la 3.
Ushindi huu umewafanya Azam FC kuipiku Mtibwa Sugar na kuongoza Ligi wakiwa Pointi 3 mbele yao lakini Mtibwa Sugar wamecheza Mechi 1 pungufu.
Mechi ijayo kwa Azam FC ni hapo Jumamosi Jijini Dar es Salaam watakapoivaa Simba.
Rashid Mandawa dakika ya 55 kipindi cha pili alifanya 2-1 na kasi ikaanza kwa Timu ya Kagera Sugar kwa kuongeza bidii ili waweze kusawazisha bao lililobaki.
Timu zikisalimiana zote mbili kati ya Kagera na Azam FC
Wachezaji wa akiba wa Kagera Sugar wakiwaangalia wenzao Uwanjani.
Mgeni rasmi wa mchezo Ligi kuu soka Tanzania Bara Kagera Sugar Vs Azam Fc, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wa pili toka kushoto) akiwa ameketi meza moja na Mwenyekiti wa MZFA Jakson Songora (wa kwanza kushoto) na viongozi wengine.
Wachezaji wa Azam Fc wakishanglia kwa kurudi Uwanjani
Mashabiki waliotoka Kagera kuja kuwaangalia wenzao wakisakata kabumbu katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza
Mashabiki
Kipa wa Azam Fc akiwapanga wachezaji wake wakati wa frii kiki
Mchezaji wa Kagera Sugar chini baada ya kuumizwa..
Mashabiki wa Kagera Sugar
Mashabiki kwenye Uwanja wa CCM Kirumba wakiutazama mpira kati ya Kagera Sugar vs Azam FC
Baada ya bao hilo, Azam FC ilitengeneza nafasi zaidi, lakini ikashindwa kuzitumia, huku Kagera wakizidi kupoteana uwanjani.
VIKOSI:
Kagera Sugar: Agatony Anthony, Benjamin Asukile, Abuu Mtiro, Eric Kyaruzi, Ibrahim Job/Shai Mpala dk57, George Kavilla, Juma Mpola, Babu Ally/Paul Ngway dk30, Rashid Mandawa, Daudi Jumanne ‘Dunga’ na Atupele Green/Adam Kingwande dk79.
Azam FC: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Said Mourad, Serge Wawa, Kipre Balou, Mudathir Yahya, Frank Domayo/Himid Mao dk53, Didier Kavumbangu/Gaudence Mwaikimba dk76, Kipre Tchetche/Amri Kiemba dk85 na Brian Majwega.

Chupuchupu!! juu kwa juu wakigombea mpira wa Kichwa.
Timu zote mbili zikiingia Uwnjani, tayari kwa mtanange.
Wachezaji wa Timu ya Azam Fc wakiingia Uwanjani CCM Kirumba tayari kwa mtanange na Wenyeji Kagera Sugar
Wachezaji wa Kagera Sugar
No comments:
Post a Comment