BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 6, 2015

MAPINDUZI CUP 2015: SIMBA YAINYUKA BAO 1-0 JKU


Mshambuliaji wa Simba Elias Maguri akijiandaa kumpiga chenga Beki wa timu ya JKU Khamis Abdallah.

Hapa hukatizi ndugu yangu!

Mshambuliaji wa timu ya Simba Ramadhani Shindano Messi akisherehekea bao lake alilofunga mnamo dakika ya 11ya mchezo wao na timu ya JKU uliofanyika uwanja wa Amaan. Simba imeshinda 1-0.

Wachezaji wa Simba wa kiwana mfungaji wa bao la kwanza Messi akiwa anasali huku wachezaji wezake wakiwa nyumba yake wakishangilia ushindi huo.

Beki wa timu ya JKU Khamis Abdallah akiokoa mpira huku mshambuliaji wa timu ya Simba akimuangalia baada ya kuukosa mopira huo na kuokolewa.

Mchezaji wa Simba na JKU wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Simba imeshinda 1--0.

Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao wakati ikicheza na timu ya JKU katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, uliofanyika uwanja wa Amaan Simba imeshinda 1--0

Mchezaji wa timu ya JKU akimpita mchezaji wa timu ya Simba wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi.

Beki wa Simba akiokoa moja ya hatari golini kwake huku mshambuliaji wa JKU akiwa tayari kuleta madhara.

Beki wa Sima Kessy Ramadhani akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa timu ya JKU Hilal Rehani, wakati wa mchezo wao wa mwisho Kombe la Mapinduzi, timu ya Simba imeshinda bao 1--0.

Mshambuliaji wa timu ya Simba Elias Maguri akijiandaa kuzuiya mpira huku beki wa timu ya JKU akijiandaa kumzuiya.

Mshambuliaji wa timu ya JKU Hilal Rehani, akimpiga chenga beki wa timu ya Simba Hassan Is-haka.
Wachezaji wa Simba na JKU wakikimbilia mpira huku mchezaji wa JKU Khamis Said, akiuwahi mpira huo na beki wa Simba Hassan Is-haka akijaribu kumzuiya.

Kipa wa timu ya Simba John Manyika akidaka mpira huku mshambuliaji wa timu ya JKU Amour Omar Janja.

Kocha Mkuu wa timu ya JKU Malale Hamsini akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wao na Simba kumalizika kwa kufungwa bao 1--0, Timu ya JKU imefanikiwa kuingia Robo fainali na kukutana na timu ya Yanga siku ya Alhamis. katika uwanja wa Amaan

Kocha Mkuu wa timu ya Simba Goran akizungumza waandishi wa habari wa michezo baada ya mchezo wao na JKU, na kusema timu ya JKU imetowa upinzani mkubwa kwa timu yake

No comments:

Post a Comment