BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 6, 2015

MAPINDUZI CUP 2015: YANGA YAITUNGUA SHABA BAO 1-0. MTUNGUAJI NI ANDREY COUTINHO!

Mshambuliaji wa timu ya Yanga kutoka Brazil akiwa na Mchezaji mwezake kutoka Laiberia wakishangilia bao
Yanga imemaliza hatua ya makundi kwa kuwa na pointi 9 baada ya kupata ushindi wa tatu mfululizo. Yanga imeifunga Shaba kwa bao 1-0 katika mechi ngumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Pamoja na kushambulia sana na kukosa sana, Yanga walilazimika kusubiri hadi dakika ya 86 wakati Andrey Coutinho alipofunga bao kwa kichwa akiunganisha krosi ya Simon Msuva. Yanga walipoteza nafasi zaidi ya tano za wazi za kufunga kupitia kwa Mrisho Ngassa, Simon Msuva na Amissi Tambwe.

No comments:

Post a Comment