BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 27, 2015

REFA MARK CLATTENBURG KUCHEZESHA MTANANGE KUKATA NA SHOKA KATI YA CHELSEA vs MANCHESTER CITY JUMAMOSI HII.

Mark Clattenburg ndie ameteuliwa kuchezesha ule mtanange wa Jumamosi Uwanjani Stamford Bridge kati ya Vinara wa Ligi Kuu England Chelsea na Mabingwa Watetezi wa Ligi hiyo Manchester City.
Chelsea wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Man City.
Refa Clattenburg ni mmoja wa Marefa Wawili wa England ambao wapo kwenye kiwango cha juu kabisa cha Urefa cha UEFA na mwingine ni Martin Atkinson.
Lakini Refa huyo ameshawahi kulalamikiwa na Klabu zote hizo mbili huko nyuma.
Bosi wa Man City, Manuel Pellegrini anaetokea Nchini Chile, ameshawahi kudai Clattenburg aliwakosesha ushindi walipotoka Sare 2-2 na Arsenal Mwezi Septemba huko Emirates na Msimu uliopita Pellegrini pia alimwandama Refa huyo wakati walipofungwa 3-2 na Liverpool.
Chelsea pia wana historia ya uhasama na Clattenburg ambae waliwahi kumsakama na kumshitaki kwa kumkashifu Kibaguzi Kiungo wao John Obi Mikel wakati wa Mechi ya Ligi dhidi ya Manchester United Mwezi Oktoba Mwaka 2012.

Hata hivyo, baadae, FA, Chama cha Soka England, kilimsafisha Refa huyo kuhusu tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment