BUKOBA SPORTS

Monday, June 29, 2015

ZINEDINE ZIDANE AWAAMSHA MAN UNITED, AITAKA ITUMIE NAFASI ILIYONAYO KUBORESHA SAFU YA ULINZI!

Lejendari wa Ufaransa, Zinedine Zidane, ambae sasa ni Kocha wa Castilla, Timu B ya Real Madrid, ameelekea kuwaamsha Manchester United baada kutaka kumchukua Kijana wao alie kwenye Timu yake kwa Mkopo.
Man United ilimnunua Guillermo Varela, mwenye Miaka 22 ambae alikuwepo Timu ya Taifa ya Uruguay iliyocheza Copa America Wiki iliyopita, Mwaka 2013 kwa Dau la Pauni Milioni 2 kutoka Klabu ya Penarol ya Uruguay na kumsainisha Mkataba wa Miaka Mitano.
Varela, ambae ni Fulbeki wa Kulia, alichezea Kikosi cha Vijana wa Man United cha U-21 na alipotua Louis van Gaal Mwaka Jana, Kijana huyo akaruhusiwa kwenda kwa Mkopo huko Castilla baada ya Zinedine Zidane kuvutiwa nae.
Zidane amezungumza: "Nilijua yupo Fulbeki wa Uruguay Man United. Niliomba kumwona na nikampenda. Kwa bahati tuliweza kumleta Real Madrid na naona atafaa sana hapa kwetu."
Maendeleo ya Varela sasa yamemgusa Louis van Gaal ambae anataka kumchukua Kijana huyo kwenye Ziara ya huko Marekani ambako watakwenda Julai 14 ili kumpima kama anaweza kuchukua namba ambayo sasa inachezwa na Winga Antonio Valencia badala ya Rafael ambae kila Siku kaumia.
Tangu astaafu Fulbeki wa Kulia Gary Neville Februari 2011, Man United haijapata Mtu barabara kwenye nafasi hiyo na imelazimika kumtumia kiraka Valencia ambae ni mzuri kwenda mbele ila kwenye Difensi ni dhaifu.

No comments:

Post a Comment