
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la John Smith's Manchester United walifungwa goli la kwanza baada ya Juan Mata kupoteza mpira ulionaswa na Aaron Mooy.
Mooy aliambaa na mpira huo na kumpasia kiungo Tom Ince aliyepiga mpira uliookolewa na kipa David de Gea, na mpira huo kumkuta Mooy akaupachika wavuni.
Uzembe wa beki Victor Lindelof uliizawadia Huddersfiel goli la pili lililofungwa na Laurent Depoitre, huku Marcus Rashford aliyetokea benchi akifunga goli pekee la Manchester United.


No comments:
Post a Comment