BUKOBA SPORTS

Wednesday, February 21, 2018

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BAYERN MUNICH YAIFUNGA BAO 5-0 BESIKTAS


Timu ya Bayern Munich imeichakaza Besiktas iliyokuwa na wachezaji 10 kwa kupata ushindi mnono wa magoli 5-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16.
Wenyeji wameshinda mchezo wao wa 14 mfululizo baada ya kuutawala mchezo huo katika kipindi cha pili dhidi ya Besiktas ambayo mchezaji wao Domagoj Vida alipewa kadi nyekundu.
Katika mchezo huo Thomas Muller alifunga magoli mawili naye Kingsley Coman akafunga goli moja huku mfungaji anayeongoza kwa magoli Robert Lewandowski akifunga mawili.


Thomas Muller akifunga goli kati ya magoli yake mawili aliyofunga jana

Mchezaji Kingsley Coman akifunga goli la pili la Bayern Munich

No comments:

Post a Comment