
Goli la kwanza Lionel Messi katika michezo tisa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya limetosha kwa Barcelona kulazimisha sare ya goli 1-1 ugenini katika mchezo wa hatua ya 16.
Chelsea walionekana kumdhibiti Messi huku Willian akiachia mashuti yaliyogonga mara mbili mwamba wa goli la Barcelona kabla ya baadaye kufunga goli.
Katika mchezo huo Barcelona haikuonekana tishio lakini alikuwa Andres Iniesta aliyemtengenezea nafasi ya kufunga Messi na kusawazisha goli.

Mbrazili Willian akiachia shuti na kufunga goli lililoifanya Chelsea iongoze

Wachezaji wa Chelsea wakiwa hoi baada ya Lionel Messi kusawazisha goli
No comments:
Post a Comment