Sunday, December 31, 2017
FULL TIME: CRYSTAL PALACE 0-0 MANCHESTER CITY

Crystal Palace licha ya kutoa sare tasa na vinara wa ligi Manchester City, pia ingeweza kuibuka na ushindi wa goli moja lakini kipa Enderson aliwanyima ushindi.
Palace walidhani kuwa wataibuka na ushindi baada ya kupata penati dakika za mwisho baada ya kuangushwa Wilfred Zaha lakini penati ya Luka Milivojevic ilipanguliwa.
Licha ya kutibuliwa rekodi ya ushindi mfululizo Manchester City pia imejikuta ikikumbwa na hofu ya majeruhi baada ya Kevin De Bruyne na Gabriel Jesus kuumia.


MANCHESTER UNITED WATOKA SARE TENA MBELE YA SOUTHAMPTON 0-0
Marcus Rashford akiendesha mpira mbele ya mchezaji wa Southampton.
Lukaku kiwa chini akiugulia jeraha.
Juan Mata
Luke Shaw akimwekea kifua Dusan Tadic
LIVERPOOL 2 vs 1 LEICESTER CITY, MOHAMED SALAH AIBEBA LIVERPOOL NYUMBANI!

Raia wa Misri Mohamed Salah amefunga magoli mawili na kuisaidia Liverpool kuongeza rekodi yao ya kutofungwa katika michezo 15 kwenye michuano yote baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Leicester City.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Anfield Jamie Vardy aliwapatia wageni goli la kuongoza akiitumbukiza kiulani pasi ya Riyad Mahrez goli lililoduma hadi kipindi cha pili pale Salah alipoisawazishia Liverpool.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri baadaye tena alimzungusha Harry Maguire na kuachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la pili na kufikisha magoli 17 katika michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu huu.

Mshambuliaji nyota wa Leicester City akifunga goli la kwanza katika mchezo huo

Mshambuliaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah akifunga goli la kusawazisha kabla ya baadaye kuongeza la pili
CHELSEA YAFUNGA MWAKA 2017 KWA KWA KUINYUKA STOKE CITY BAO 5-0, WAPANDA NAFASI YA PILI

Katika mchezo huo wenyeji Chelsea walifunga goli la kwanza kupitia kwa Antonio Rudige kufuatia krosi ya Mbrazil Willian kisha baadaye Danny Drinkiwater akaongeza goli la pili kisha Pedro akafunga la tatu.
Willian aliongeza goli la nne kwa mkwaju wa penati baada ya kuchezewa rafu na Geoff Cameron na katika dakika ya 88 Zappacosta akakamilisha karamu ya magoli kwa kufunga goli lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza.


Danny Drinkwater akifunga kwa shuti la kuubetua mpira kwenye kona ya goli.
Friday, December 29, 2017
KOCHA ARSENE WENGER HANA WASIWASI YA KUMKOSA SANCHEZ ANAYEONDOKA JANUARI, WASHINDA BAO 3-2 DHIDI CRYSTAL PALACE.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema kuwa hana wasiwasi wa kumpoteza Alexis Sanchez Januari licha ya mshambuliaji huyo kufunga mara mbili wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Crystal Palace.
Crystal Palace ilisawazisha goli kupitia kwa Andros Townsend baada ya Shkodran Mustafi kufunga goli la kwanza katika mchezo huo na kisha baadaye katika kipindi cha pili akafunga mawili kwa muda wa dakika nne.
Crystal Palece ilipata goli la pili katika kupitia kwa James Tomkins kwa mpira wa kichwa, hata hivyo walishidwa kusawazisha la tatu na kuifanya Arsenal iliyokatika nafasi ya sita kuwa na pinti sawa na Tottenham iliyonafasi ya tano.



WASANII ASLAY NA NANDY WATUA BUKOBA LEO HII, TAYARI KWA SHOW YA MIAKA 9 YA KASIBANTE REDIO KWENYE UKUMBI WA ST. THEREZA KESHO 30/12/2017
Kesho Jumamosi wanatarajiakuangusha bonge la show kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba pale ukumbi wa St.Theresa karibu na banki ya NMB.
Show hiyo ni moja ya maadhimisho ya miaka 9 ya uwepo wa Kasibante Fm Radio Bukoba tangu kuanzishwa kwake.
Show hiyo itaanza majira ya saa moja jioni hadi majogoo huku Wheel Steel ikisimamiwa na DJ`s kutoka Pro24Tanzania.
Wednesday, December 27, 2017
CONTE ASEMA KUKOSA BAHATI KUMEWAFANYA WASHINDWE KUWAFIKIA MAN CITY, MAN UNITED SARE TENA!

Chelsea imepata ushindi wa sita mfululizo katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya jana kusakata kandanda safi na kupata magoli hayo kupitia kwa Alvaro Morata na Marcos Alonso.

Alvaro Morata akifunga kwa mpira wa kichwa goli la kwanza la Chelsea

Katika mchezo huo Ashley Barnes aliwafungia wageni goli la kwanza na kisha baadaye Steven Defour akafunga goli la pili na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa 2-0.

FIRMINO AFUNGA MAWILI WAKATI LIVERPOOL IKICHAPA BAO 5-0 SWANSEA FC

Roberto Firmino amefunga magoli mawili wakati Liverpool ikiichapa Swansea isiyonakocha na iliyomkiani kwa magoli 5 bila majibu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza Katika mchezo huo Philippe Coutinho alifunga goli la kwanza baada ya kunasa pasi ya Mohamed Salah, kabla ya Firmino kufunga la pili na Trent Alexander-Arnold la tatu.
Roberto Firmino aligongeza goli la tatu kisha baadaye Oxlade-Chamberlain akamalizia karamu ya magoli kwa kufunga goli la tano.

Roberto Firmino akimalizia kiulaini pasi iliyozaa goli ya Mohamed Salah

Oxlade-Chamberlain akiachia shuti na kufunga goli la tano katika mchezo huo
Monday, December 25, 2017
ROBERTO FIRMINO AIOKOA LIVERPOOL DAKIKA ZA MWISHO NA KUTOKA SARE NA ARSENALYA GOLI 3-3

Goli la shuti kali la Roberto Firmino limeisaidia Liverpool kutoa sare katika mchezo mzuri wa Ligi Kuu ya Uingereza ulioshuhudia Arsenal ikifunga magoli matatu ndani ya dakika tano za kipindi cha pili.
Arsenal ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Philippe Coutinho aliyefunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa kabla ya raia wa Misri Mohamed Salah kuongeza goli la pili katika kipindi cha pili.
Lakini hafla Arsenal walizinduka na kufunga goli la kwanza kupitia kwa Alexis Sanchez akifunga kwa mpira wa kichwa krosi ya Hector Bellerin, kabla ya Granit Xhaka kutumbukiza la pili kisha Mesuit Ozil kufunga la tatu.

Philippe Coutinho akifunga goli kwa mpira wa kichwa hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kufunga goli kwa mpira wa kichwa katika Ligi Kuu ya Uingereza

Mohamed Salah akifunga goli la pili la Liverpool kwa shuti lililomshinda kipa wa Arsenal

Alexis Sanchez akiifungia Arsenal goli la kwanza lililoamsha ari ya kusawazisha magoli waliyofungwa na kuongeza moja

Roberto Firmino akiisawazishia Liverpool goli la tatu na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya magoli 3-3
Subscribe to:
Posts (Atom)