BUKOBA SPORTS

Wednesday, January 31, 2018

UHAMISHO: AUBAMEYANG AKAMILISHA KUHAMIA ARSENAL

Pierre-Emerick Aubameyang poses in Arsenal's home kit after completing his transfer from Borussia DortmundNi rasmi Pierre-Emerick #Aubameyang sasa ni mchezaji wa Arsenal, klabu hiyo ya London kaskazini imetangaza.

Aubameyang ametia saini mkataba wa "muda mrefu kwa uhamisho ambao umevunja rekodi ya klabu" kutoka Borrussia Dortmund.
Arsene Wenger shakes hands with Aubameyang to welcome him to Arsenal - he has joined for a new club-record fee of £56m"Mchezaji wetu wa pili wetu kumnunua wakati wa kipindi cha kuhama wachezaji Januari. Auba ni miongoni mwa washambuliaji stadi zaidi duniani. Amefunga mabao 98 katika mechi 144 akichezea klabu ya Dortmund ligi ya Bundesliga na amesaidia ufungaji wa mabao 172 katika mechi 213 ambazo ameshiriki akichezea klabu hiyo yake ya zamani michuano yote," Arsena wameandika kwenye mtandao wao.
Dortmund ilikuwa imesema kuwa itamuuza mcheza huyo baada ya kupata mbadala wake huku mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo.
Aubameyang clutches the club badge on his chest in a display that will endear him to Arsenal fans alreadyAubameyang alifunga mabao 141 katika mechi 213 akiichezea Dortmund tangu 2013, ikiwemo mechi 21 kati ya 24 msimu huu.

Lakini alipigwa marufuku na klabu hiyo ya Ujerumani katika mechi yao dhidi ya Wolfsburg tarehe 14 Januari kwa kukosa mkutano wa timu.
Gabon striker Aubameyang scored 141 goals in 212 appearances for Borussia DortmundMshambuliaji huyo pia aliwachwa nje kwa mechi yao dhidi ya Hertha Berlin kwa sababu maafisa wa klabu hiyo walihisi hakuwa na malengo lakini alicheza dakika 90 katika mechi ya Jumapili dhidi ya Freiburg.
Ameichezea Gabon mara 56 akifunga magoli 23.

Monday, January 29, 2018

LA LIGA: LIONEL MESSI AIPATIA USHINDI TIMU YA BARCELONA BAO 2-1 DAKIKA ZA LALA SALAMA.


Mchezo wa kwanza wa Philippe Coutinho katika La Liga akiwa na Barcelona umemalizika kwa ushindi wa magoli 2-1 baada ya Barcelona kutokea nyuma na kuifunga Alaves.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City John Guidetti aliandika goli la kwanza kwa mpira uliomshinda kipa Marc-Andre ter Stegen na kuwafanya wageni Alaves waongoze.
Luis Suarez aliisawazishia Barcelona goli hilo na kisha baadaye Lionel Messi kuihakikishia ushindi kwa goli la mpira wa adhabu.


Mpira wa adhabu uliopigwa na Lionel Messi ukielekea kuwapita mabeki na kujaa wavuni.

MANCHESTER CITY NA CHELSEA ZASHINDA MECHI ZA KOMBE LA FA

Manchester City imetinga kilaini katika raundi ya tano ya Kombe la FA kwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya timu ya Cardiff City.
Kevin de Bruyne aliipatia Manchester City goli la kwanza katika kipindi cha kwanza na Raheem Sterling akaongeza la pili kipindi cha pili.
Mpira uliopigwa na Kevin de Bryune ukitinga wavuni na kuandi goli la kwanza
Kocha Antonio Conte amemuelezea Michy Batshuayi kama mchezaji kijana mwenye fursa ya kung'ara baada ya kufunga magoli mawili, Chelsea ikishinda magoli 3-0 dhidi ya Newcastle.

Mshambuliaji huyo Mbelgiji amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha Conte, ambaye alisema mchezaji huyo anaweza kuondoka kwa mkopo mwezi huu. Marcos Alonso alifunga la tatu.
Mchezaji kijana wa Chelsea Michy Batshuayi akifunga goli kwa kuupiga mpira kwa kuubetua

WEST HAM YAIFUNGA LIVERPOOL KATIKA MCHEZO WA KOMBE LA FA BAO 3-2


Jay Rodriguez amefunga magoli mawili wakati West Brom ikiishinda Liverpool kwa magoli 3-2 katika mchezo wa Kombe la FA raundi ya nne uliotawaliwa na maamuzi ya kutumia msaada wa video.
Refa Craig Pawson alikataa goli la Albion, akaipa Liverpool penati na kuchelewa kwa dakika tatu kufanya maamuzi ya kuwapati goli West Ham goli la tatu hadi aliposaidiwa na refa anayetumia picha za video.
Rodriguez alifunga goli la kusawazisha baada ya Firmino kuifungia Liverpool goli la kuongoza, na kisha tena Rodriguez akaongeza goli la pili na kufanya matokeo kuwa 2-1. Joel Matib alijifunga goli la tatu baadaye Mohamed Salah akafunga goli la pili la Liverpool.


Kipa wa West Ham Ben Foster akimdhibiti Mohamed Salah kufunga goli

Refa Craig Pawson akiomba msaada wa refa wa video baada ya kushindwa kufanya maamuzi

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akiwa amechanganyikiwa na kipigo kutoka kwa West Ham

EMMANUEL OKWI NA BOCCO WAIPA SIMBA USHINDI, KWASI NAYE NI HABARI NYINGINE

VINARA wa Soka Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC, leo imezidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 15 na kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa pointi tano zaidi ya Azam FC iliyopo nafasi ya pili. Yanga ambayo juzi iliifunga Azam, ni ya tatu ikiwa na pointi 28.

Simba ilipata bao la kuongoza lililofungwa na John Bocco katika dakika ya 17 baada ya kuunganisha wavuni kona na Shiza Kichuya.
Bocco alifunga la pili katika dakika ya 26 akimalizia kwa kichwa krosi ya Said Ndemla.

Majimaji walinyimwa penalti ya wazi katika dakika ya 19 baada ya Juuko Murshid kumchezea rafu, Geofrey Mlawala lakini mwamuzi akasema ipigwe adhabu ndogo.

Timu hiyo ya Songea ilizinduka na kujaribu kutengeneza nafasi mbili baada ya kulifikia lango la Simba, lakini walishindwa kufunga.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko, ambapo ilimtoa Murshid na kumuingiza James Kotei, na kuongeza kasi kwa timu hiyo.
Emmanuel Okwi aliiongezea Simba ushindi baada ya kufunga bao la tatu katika dakika ya 52 baada ya mabeki wa Majimaji kushindwa kuokoa mpira wa kona uliochongwa na Kichuya.

Okwi alifunga bao la nne likiwa la pili kwake katika dakika ya 68 akipokea pasi safi ya Bocco, ambaye alifanya kazi ya ziada kuwatoka mabeki wa Majimaji kabla ya kutoa pasi kwa mfungaji.

Okwi ameendelea naye kuzidi kujichimbia kileleni katika mbio za kusaka kiatu cha dhahabu baada ya kufikisha mabao 12 hadi sasa.
Vikosi vilikuwa;Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Juuko Murshid/James Kotei, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Emannuel Okwi, Said Ndemla, John Bocco, Shiza Kichuya/Laudit Mavugo na Jamal Mnyate.

Majimaji: Salehe Malande, Lucas Kikoti, Mpoki Mwakinyuke, Kenned Kipepe, Paulo Maona, Hassan Hamisi, Peter Mapunda, Yakubu Kibiga, Geofrey Mlawa/Six Mwasekaga, Maccel Bonaventure na Jafar Mohamed.
Katika mchezo mwingine, Singida United jana walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

CRISTIANO RONALDO AFUNGA MAGOLI MAWILI KWA PENATI


Cristiano Ronaldo amefunga mikwaju ya penati miwili katika kipindi cha kwanza na kuisaidia Real Madrid kuifunga Valencia magoli 4-1 na kupunguza presha ya kutimuliwa kocha wao Zinedine Zidane.
Ushindi huo unaifanya Real Madrid kupunguza pengo lake na wenyeji Valencia kuwa tofauti ya pointi mbili tu, ikiwa na mchezo mmoja mkonono, ingawa bado ipo nyuma kwa pointi 16 na vinara wa La Liga Barcelona.
Valencia ilipata goli lake pekee kupitia kwa Santi Mina, huku magoli mengine ya Real Madrid yakifungwa na Marcelo na Toni Kroos kufunga goli la nne kwa shuti kali la masafa dakika moja kabla ya mpira kumalizika.


Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo akifunga goli kwa mkwaju wa penati

Mjerumani Toni Kroos akiachia shuti kali na kufunga goli katika dakika ya 89

YANGA YAIFUNGA AZAM FC NYUMBANI KWAO

YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Aidha, mchezaji wa Azam FC Abubakari Salum ‘Sure boy’ alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumsukuma Hassan Kessy mbele ya mwamuzi wa kati Israel Nkongo.
Azam ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la uongozi dakika ya tatu baada ya kuanza kwa mchezo huo likifungwa na Shaban Chilunda huku Obrey Chirwa akisawazisha dakika ya 30 na la ushindi likifungwa na Gadiel Michael.
Ushindi huo umeendelea kuibakiza Yanga katika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikifikisha jumla ya pointi 28, nyuma ya Azam yenye pointi 30 na Simba 32.

Azam FC ilianza mpira kwa kasi na kufanikiwa kupata bao hilo la uongozi baada ya Chilunda kutengenezewa pasi na Bruce Kangawa.
Baada ya Azam kuongoza bao hilo walianza kupunguza kasi na kuwapa nafasi wapinzani wao kusawazisha kupitia kwa Chirwa aliyepata pasi ya Ibrahim Ajibu ambapo alimzunguka kipa Razaki Abalora na kufunga.
Azam baada ya kusawazishiwa walirudi tena kwenye kasi na kufanya mashambulizi mengi lakini hayakuzaa matunda, na kutoa nafasi zaidi kwa Yanga kujiamini ambapo Gadiel alipiga shuti kali nje ya 18 na kuifungia Yanga bao la pili.


Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Azam ilikuwa ikiongoza kwa mashambulizi lakini Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili Azam iliendeleza kasi ya mashabulizi bila mafanikio kwani tayari Yanga iliweka ukuta na kupata wakati mgumu wa kufunga. Hadi mpira unakwisha matokeo hayo
Kocha wa Azam alijaribu kufanya mabadiliko kadhaa lakini hayakuzaa matunda. Dakika 36 alimtoa Bernard Arthur na kumuingiza Salmin Hoza, pia, kipindi cha pili dakika 55 na 65 alimtoa Stephen Kingue na Shaban Chilunda na kuingia Mbaraka Yusufu na Paul Peter.
Kwa upande wa Yanga dakika ya 66 iliwatoa Emmanuel Martin na kuingia Geofrey Mwashiuya, pia, dakika 68 alimtoa Ibrahim Ajibu na kuingia Juma Mahadhi.
Azam FC.Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Agrey Morris, Yakubu Mohamed, Stephan Kingue, Salum Abubakari, Joseph Mahundi, Bernard Arthur, Shaban Chilunda na Enock Atta.
Kikosi cha Yanga. Youthe Rostand, Kelvin Yondani, Gadiel Michael, Hassan Kessy, Raphael Daud, Andrew Vicent, Said Juma, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin.
Mechi nyingine zilizochezwa ni Mwadui dhidi ya Njombe waliopata sare ya mabao 2-2 na Mbeya City dhidi ya Mtibwa sare ya bila kufungana 0-0. Na Kagera Sugar na Lipuli pia zikitoka sare ya 0-0.

Thursday, January 25, 2018

MSIMU MBAYA WAREAL MADRID WAENDELEA...WAKIWA KWAO WAKUBALI KICHAPO CHA BAO 2-1 NA LEGANES

Kiwango duni cha Real Madrid katika msimu huu kimezidi kuisakama timu hiyo baada ya kutolewa katika michunano ya kombe la Copa del Rey baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Leganes katika dimba la Bernabeu.
Mabingwa hao wa Ulaya walikuwa wanaongoza kwa matokeo ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Leganes katika mchezo wa kwanza.
Madrid midfielder Isco shows quick feet to retain possession under pressure from two playersJavier Eraso alifunga goli la kwanza katika mchezo wa pili na kufanya jumla ya matokeo kuwa sare, lakini baadaye Karim Benzema akafunga na kuifanya Real iongoze kwa matokeo ya ujumla.
Laganes walipata ushindi kupitia goli la Mbrazili Gabriel hit Leganes na kuwafanya wageni hao kusonga mbele hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa goli la ugenini. Mpaka dakika zinamalizika 90 kwenye Uwanja huo Real Madrid 1-2 Laganes.
Mshambuliaji Karim Benzema akifunga goli pekee la Real Madrid katika mchezo huo

CARABAO: ARSENAL 2 vs 1 CHELSEA, BLUES WATUPWA NJE! SASA FAINALI NI MAN CITY USO KWA USO NA ARSENAL


Kocha Arsene Wenger amesema kikosi chake kinacheza kwa ufasaha kufuatia kuondoka kwa Alexis Sanchez, baada ya Arsenal kutokea nyuma na kuifunga Chelsea magoli 2-1 katika kombe la Carabao, na kutinga fainali dhidi ya Manchester City.
Nacho Monreal, whose initial header sparked a double deflection off Marcos Alonso and Rudiger, wheels away to celebrateBaada ya timu hizo kutoka sare tasa katika mchezo wa kwanza Eden Hazard aliifanya Chelsea kuongoza kupata goli lakini goli la kujifunga la Antonio Rudiger likasawazisha na kisha Granit Xhaka akafunga goli la ushindi.

Ushindi huo umekuja ikiwa ni siku mbili tu kupita tangu mshambuliaji wake nyota Sanchez kuhamia Manchester United wakibadilishana na Henrikh Mkhitaryan ambaye Manchester United imemtoa ili kufanikisha dili.
Eden Hazard akiifungia Chelsea goli la kuongoza katika mchezo huo
Granit Xhaka akifunga goli la ushindi la Chelsea kwa mpira wa kuubetu.

Wednesday, January 24, 2018

BAADA YA KAGERA SUGAR KUPOTEZA DHIDI YA SIMBA SC, WAJIPANGA KUWAFUNGA LIPULI WIKIENDI HII VPL.

SANCHEZ NA THIERRY HENRY WAWAKANA MASHABIKI WA ARSENAL

Ikiwa asilimia kubwa ya mashabiki wa Arsenal wanaamini kuwa mshambuliaji wao wa zamani Thierry Henry ndiye aliyemshawishi aliyekuwa mshambuliaji wao, Alexis Sanchez kuhamia Manchester United, hatimaye wawili hao wamekanusha taarifa hizo.
Thierry Henry ndiye aliyekuwa wa kwanza kukanusha uvumi huo unaonezwa na mashabiki wa Arsenal ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter alitweet kwa kusema “Ninajua sihitaji kuelezea hili kwa mashabiki wengi wa Arsenal lakini kinyume na uvumi hakuna muda wowote nilimwambia Alexis Sanchez aondoke Arsenal. Sikujua kwamba angeenda kusajiliwa na Man Utd mpaka nilipoona kwenye habari kama wengine.”

Baadaye naye Sanchez kupitia ukurasa wake wa Twitter alikazia ishu hiyo kwa kuandika “Nataka kufafanua kwamba Henry hakuniambia kamwe kuondoka kwenye klabu hiyo (Arsenal), bali yalikuwa ni maamuzi yangu binafsi, Anaipenda klabu na siku moja itakuwa vizuri nikimuona kama kocha wa arsenal kwa sababu anaipenda klabu“.

Sanchez amejiunga na klabu ya Manchester United kwa kubadilishana na Henrikh Mkhitaryan kutokea Manchester United kwenda Arsenal.

WENGER: TUNAMSAKA PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo inataka kumnunua mchezaji wa Borussia Dortmund mzaliwa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.
Wenger amewaambia wanahabari Uingereza kwamba mazungumzo yanaendelea kati ya Gunners na klabu hiyo ya Bundesliga.
Wanahabari walimwuliza Wenger iwapo ana imani kwamba watafanikiwa kumnunua mshambuliaji huyo ambaye amekuwa akitafutwa na klabu nyingi.

Aliwajibu: "Kuwa na imani au kutokuwa na imani, sijui. Kwa sasa, hatujakaribia kutia saini mkataba wowote, iwe ni kumhusu Aubameyang au mtu mwingine yeyote. Huwezi ukajua umekaribia (kumchukua mchezaji) kiasi gani."
Wenger alikuwa anazungumza na wanahabari Jumanne kabla ya mechi ya Kombe la Ligi (Carabao) Jumatano dhidi ya Chelsea.
Kufikia sasa msimu huu Aubameyang amefunga mabao 13 katika mechi 15 alizocheza.

Alifunga mabao 31 katika mechi 32 msimu uliopita na kwa sasa amepungukiwa na mabao mawili pekee kufikisha mabao 100 aliyoyafunga tangu atue Ujerumani mwaka 2013.

Duru Ujerumani zinasema itawagharimu Arsenal zaidi ya £50m kumtoa mchezaji huyo Borussia Dortmund wakifanikiwa.

Ijumaa wiki iliyopita, mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc alisema Wenger aliwakosea heshima kwa kuzungumza hadharani kumhusu mchezaji huyo.
Wenger alisema nyota huyo wa Gabon anaweza "kuingia sawa" katika klabu ya Arsenal.

Klabu hizo zinaendelea na mazungumzo ambayo huenda yakaifanya Arsenal kuvunja rekodi yake ya ununuzi wa wachezaji, ambao inashikiliwa na ununuzi wa Alexandre Lacazette kwa £46.5m.

Kando na uchezaji, Aubameyang anafahamika sana pia kwa utukutu wake.
Ameachwa nje ya kikosi cha Dortmund mara mbili msimu huu kutokana na utovu wa nidhamu.
Hakurudi kucheza kikosini Ijumaa kama ilivyotarajiwa klabu yake ilipotoka sare ya 1-1 na Hertha Berlin.

Kwa mujibu wa mwandishi wa michezo wa BBC David Ornstein, Arsenal wana imani kwamba watafikia makubaliano katika kipindi cha wiki moja ijayo kuhusu ada ya uhamisho wake na kwamba huenda wakamtoa mchezaji mmoja wao.

Arsenal wakifanikiwa kumchukua Aubameyang, basi huenda wasiwanunue wachezaji wengine kipindi hiki.
Walikuwa miongoni mwa klabu zilizokuwa zinashindania kumnunua beki wa West Brom Jonny Evans.

SIMBA SC WAJINOA UWANJA WA BANDARI

Kocha mkuu wa Simba SC, Pierre Lechantre katikati na kushoto ni kocha Msaidizi Masoud Djuma wakipeana maelekezo katika mazoezi hayo kulia ni Meneja wa Simba SC, Robert Richard Uwanja wa Bandari Temeke Jijini Dar es Salaam.Wachezaji SimbaSc wakiwa kwenye mazoezi ya kujifua kukabiliana na mchezo wao wa raundi ya 16 dhidi ya Wanalizombe MajimajiFc utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili hii majira ya Saa 10 jioni.Mchezaji wa Simba SC, Shomari Kapombe akifanya mazoezi ya kujifua kwa akili ya mchezo wao wa raundi ya 16 dhidi ya MajimajiFc yenye makzi yake Mkoani Ruvuma leo katika Uwanja wa Bandari uliopo Jijini Dar es Salaam.

AZAM FC YAJIPANGA KUCHUKUA POINT TATU KWA YANGA

Na Agness Francis
MCHEZO kati ya Timu ya Azam FC dhidi ya Timu ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Timu ya Azam imesema kuwa Timu imeishaingia Kambini kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo.Akizungumzia kuelekea kuhusu mchezo huo Afisa Habari wa Azam FC, Jaffary Iddy Maganga amesema kuwa kikosi cha Azam FC iko imara katika kuweza kuwakabili Yanga na matokeo ya mchezo huo ni Dakika 90.Azam watashuka dimba ni siku hiyo dhidi ya YangAfricans mchezo utakaokuwa wa kukata na shoka ambapo timu zote mbili zitakuwa na hamu ya kupata Ushindi wa pointi Tatu siku hiyo."Baada ya Timu kurejea kutokea Jijini Mbeya ambapo tulikokuwa na mchezo wetu na Tanzania Persons jana imeingia kambini na kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi dhidi ya YangAfrica. Mchezo huo utakuwa ni mgumu ukizingatia Yanga nayo ni timu nzuri na Ina kikosi kipana lakini na sisi tumejipanga kunyakua pointi Tatu zenye ushindi wa mabao" Amesema MagangaMpaka sasa hivi Azam FC anashika nafasi ya pili kwa kwa pointi 30 kwenye misimamo Tanzania Bara akifatiwa na mabingwa watetezi YangAfrica mwenye pointi 25, huku wakiingozwa na pointi 33 za timu ya Simba.Afisa Habari wa AzamFc, Jafari Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu kuanza rasmi jana mazoezi kule Chamazi Complex, leo katika ofisi zao zilizopo Mzizima Jijini Dar es Salaam.

JOHN BOCCO AONGOZA KWA KUMFUNGA KIPA JUMA KASEJA!

John Bocco akimtoka mchezaji wa Kagera Sugar FakhiNahodha wa klabu ya Simba John Raphael Bocco ni moja ya wachezaji wakongwe nchini kwasasa kutokana na kucheza Ligi kuu Tanzania Bara kwa muda mrefu akiwa na kikosi cha Azam Fc kabla ya kutua Simba.
Bocco ambaye amekuwa ni mchezaji mwenye hatari zaidi kwasasa kunako klabu ya Simba Jumatatu aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-0.

Mara baada ya kumfunga goli golikipa wa Kagera Juma Kaseja Bocco ameweka rekodi ya kumfunga Golikipa huyo mabao 10 na kuwa ni mshambuliaji pekee wa Tanzania aliyewahi kufanya hivyo.

Bocco amekuwa akimfunga Kaseja toka akiwa klabu ya Simba wakati huo Bocco akiitumikia Azam Fc na mara nyingi ndiye mchezaji pekee ambaye anamuumiza kichwa Juma Kaseja kutokana na kumfunga mara nyingi.

Jumatatu aliisaidia Simba kuondoka na alama tatu kwa bao la dakika ya 79 kwa pasi safi ya Sbomari Kapombe baada ya Saidi Ndemla kuifungia Simba bao la kwanza dakika ya 72.

Mbali na mchezo huo Singida wakiwa ugenini mkoani Ruvuma wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji Fc bao la Singida likifungwa na Papy Kambale dk 28 kabla ya winga hatari wa majimaji Peter Mapunda kuisawazishia Majimaji dakika ya 85 na kufanya matokeo kuwa 1-1

NMB YAINGIA MKATABA MWINGINE NA AZAM FC


Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdul Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkurungezi Mkuu wa NMB, Imeko Bussemaker moja ya jezi zinazotumiwa na klabu hiyo msimu huu.

Klabu ya Azam FC imeendelea kuingia kwenye neema mpya baada ya kuingia tena mkataba mpya wa Benki ya wazalendo ya NMB.

NMB wanaonekana kufurahishwa na mambo yalivyokwenda katika mkataba wao wa kwanza na NMB baada ya kuonekana kuutendea haki mkataba wao wa awali wa benki hiyo hivyo imewaongezea mwingine wa mwaka mmoja ambao utawasaidia kupambana kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Akizungumza wakati wa kusainishana mkataba huo Mkurungezi wa NMB, Imeko Bussemaker, alisema kwamba wameamua kuingia mkataba mpya na Azam FC.

Bosi huyo ameweka wazi namna ambavyo wamevutiwa na Azam FC na namna walivyoheshimu mkataba wao.
Wanaamini Azam itaongeza wigo mkubwa katika kuzalisha wachezaji wachanga hapa nchini ambao wataiinua hata timu ya taifa wanayoidhamini pia.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, yeye amewashukuru NMB kwa udhamini huo “Niwashukuru sana kwa hili lakini huku napenda niwaahidi kua siku chache zijazo nitarudi hapa tena kuwakabidhi Kombe la Ligi Kuu Bara.

"Kwani tunaamini hadi mwisho wa msimu mambo yatanyooka maana farsafa yetu kwa sasa tunaendelea kupambana kimyakimya kama tunamfukuza mwizi,” alisema Abdul.


Mkurungezi wa NMB,Imeko Bussemaker (kushoto),akikabidhi mkataba huo kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdul Mohamed ndani ya makao makuu ya ofisi hizo Posta jijini Dar es Salaam, mapema leo.

Nahodha wa timu ya Azam FC, Himidi Mao (kushoto), akimkabidhi kombe lao waliloshinda kwenye michuano ya mapinduzi Cup Mkurungezi Mkuu wa NMB,Imeko Bussemaker baada ya shughuli za kusainishana mkata mpya kumalizika.

Mkurungezi Mkuu wa NMB,Imeko Bussemaker (kushoto), akisaini mkata huo sambamba na Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdul Mohamed.

Baadhi ya wanahabari wakitekeleza wajibu wao wakati wa makabidhiano ya mkataba huo.

Wakurugezi na baadhi ya wafanyakazi wa NMB,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiana mkataba huo.